Sumaye haeleweki anachosimamia


Yeye Sumaye, Lowassa, Mbowe, Mtei, Ndesamburo, Mengi, Bakhressa, Manji, na wengine wengif tu walifanikiwa vipi chini ya huo mfumo wa CCM ambao Sumaye anaukosoa?
 
huyu jamaa amejidhalilisha sana,amekuwa icon ya unafiki na uchu wa madaraka,atajuta sana baada ya october

MTU anapoomba kuleta uongozi mbadala anajua kuna kushindwa Na kushinda,kwa mtazamo huu was mleta mada eti MTU anayejaribu kufanya hivyo anamuona msaliti, mjinga Na eti atakuwa na maisha magumu baada ya uchaguzi akishindwa, kwa mtizamo huu itaichua Tanzania miaka 1000 kupiga hatua. Na kwa kweli hili linaelezea kiwango cha ujinga cha mleta mada
 
Mpaka sasa katika timu zote za Wagombea anayeshusha nondo nzuri ni Bwana F.Sumaye,sio kama watu wengine kwenye Kampeni eti nivue shati nisivueeeee!!!!Kifimbo oyeeeee!!!.CCM OUT

Enzi zetu tulipokuwa vijana kama huyu
hatukuwahi kuwa mashabiki wa majambazi kama sumaye
sio wakushabikiwa kabisa
n hatari sana kwa taifa hili
 
Kuhusu Sumaye na hata Lowassa, CCM wasipoteze muda kulalamika kuwa hawa hawastahili kuwakosoa eti kwa vile walikuwa nao muda mrefu tena walikuwa mawaziri wakuu. Hoja ya aina hiyo inazidi kudhihirisha jinsi CCM ilivyo tatizo kuu hapa nchini. Ndio maana hata Magufuli anasota kujinadi kibinafsi (chagua Magufuli; chagua mtu sio chama; maendeleo hayana chama!). For sure the party has become a serious liability!

Kama waingereza wasemavyo, akina Sumaye wanaionjesha CCM ladha ya dawa waliyoitengeneza wenyewe - a taste of their own medicine. Chama na serikali makini vinawezaje kuwa na Waziri Mkuu zero na mwingine kufikia wadhfa wa fisadi mkuu miaka yote hiyo vikiwa kimya kabisa. Wakati wananchi na vyama vya upinzani hasa CHADEMA vikipigia kelele ufisadi, wao CCM waliendeleza jeuri ya kupuuza "kelele za mlango". Sasa mlango umebanduka jamaa ndio wanazinduka eti leo wamehamia upande wa kupiga vita ufisadi! What hypocrisy!

CCM has to go, simple. Watanzania wakipoteza fursa hii adhimu ya kuitoa CCM madarakani na kuruhusu mfumo wa kweli wa demokrasia ya vyama vingi ufanye kazi yake ipasavyo, basi wasije kumlaumu mtu yeyote kwa muendelezo wa madhila yatakayowasibu kutokana na jeuri na kibri cha ukiritimba wa chama Kimoja.
 
Yeye Sumaye, Lowassa, Mbowe, Mtei, Ndesamburo, Mengi, Bakhressa, Manji, na wengine wengif tu walifanikiwa vipi chini ya huo mfumo wa CCM ambao Sumaye anaukosoa?

Ni wazi kuwa walifanikiwa kutokana na mfumo huo kutokuwa wa haki na unaoneemesha ufisadi. Huo ndio mfumo walioamua kuusaliti leo hii. Ni wakati wa CCM kujuta kulea wasaliti hao hadi wamefikia hatua ya kukiletea chama kashkash kiasi hiki. Hili ni somo muhimu. Wenzenu wanasema there is no honour among thieves.
 

Tamaa nilianza kuiona kwa sumaye
pale alipokaribia kustaafu
Akafosi na akafanikiwa kujiongezea posho na marupurupu ya wazir mkuu atakapostaafu
 
Magufuli akiingia tu atarudisha mashamba yote kwenye vijiji...bwana zero ajipange kudadeki...
 
Mpaka sasa katika timu zote za Wagombea anayeshusha nondo nzuri ni Bwana F.Sumaye,sio kama watu wengine kwenye Kampeni eti nivue shati nisivueeeee!!!!Kifimbo oyeeeee!!!.CCM OUT

Kama Sumaye ndio mnayemuona anashusha Nondo basi Ukawa mmeshindwa asubuhi na mapema na hamna timu ya kampeni
 
huyu jamaa amejidhalilisha sana,amekuwa icon ya unafiki na uchu wa madaraka,atajuta sana baada ya october

Anasaidia harakati za kuleta mabadiriko , kumtoa mkoloni CCM madarakani. Sasa ni kipi ambacho hujamuelewa?
 
wewe unadhani Sumayi ni mpuuzi kama wewe mleta mada,awe ndani ya ccm asiwe baada ya uchaguzi,still anapata pension zake kama waziri mkuu mstaafu haijalishi yupo wapi,maisha yake yanaendelea,wewe usie jitambua ndo unamatatizo.
 
huyu jamaa amejidhalilisha sana,amekuwa icon ya unafiki na uchu wa madaraka,atajuta sana baada ya october

Kusaidia ukombozi ni kujidhalilisha? mwacheni Sumaye awapiganie wanyonge .Binafsi nampongeza sana kw kujitenga na wanafiki.
 
Eti amehamia upinzani kwa kuwa hawana safu yenye uzoefu na makini kiuongozi,huyo ndio Sumaye katika ubora wake.Hivi ana jambo gani la kujivunia alilofanya kwenye uongozi wake katika nchi hii kushawishi hadhira kuwa ni kiongozi bora.For me he is a bogus one.
 

Wakati mwingine hata takukuru tunawalaumu bure...hebu fikiria cabhatica akuajiri kutafuta na kukamata wezi wa mali ya umma, katika upelelezi wako unagundua cabhatica ni sehemu ya huo mtandao wa wizi, utafanyaje? Ukizingatia unahitaji kuishi vizuri na una majukumu mengi tu ya kifamilia.

Bila kuweka msingi wa sheria mama (katiba) utakobadili mfumo wa utendaji ulivyo sasa, hata malaika angekuwa ndiyo mkurugenzi wa pccb bado shida itakuwa palepale. Tunahitaji mabadiliko ya kweli siyo ya kuimba kwenye majukwaa!
 
huyu jamaa amejidhalilisha sana,amekuwa icon ya unafiki na uchu wa madaraka,atajuta sana baada ya october

elimu elimu elimu
sumaye ana uchu wa madaraka anagombea udiwani, ubunge au Urais? Yule ni MTU mwenye nia njema na taifa, hatajuta daima na atakumbukwa.
Hao waliobaki ccm hawana uchu wa madaraka eti e?
 

Mgombea wenu mwenyewe analaumu na kushangaa sasa hapo cha ajabu nini? semeni tu hamjui nchi inaendeshwaje mnambwelambwela tuuuu
 
Sio wewe tu mtoa mada ambae huelewi, hata Jakaya hajaelewa bado.
It's a complicated movie without subtitles...hard for pro CCM to understand.
However October 25 utaelewa, ukishindwa kuelewa utaona, usipoona utasikia.

TO HELL CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…