Sumaye awakaanga Magufuli na mkuu wa mkoa wa Dar

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema Rais John Magufuli amesahau kama amechaguliwa na wananchi jambo linalomfanya kufanya maamuzi yake bila kujali hisia zao, anaandika Hamisi Mguta.

Sumaye alitoa kauli hiyo leo alipozungumza na wanahabari katika ofisi za Kanda ya Pwani za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar es Salaam,kufuatia kauli za Rais Magufuli alizotoa jana kuwa, haelekezwi kufanya mambo yake kwani alichukua fomu peke yake, hivyo hakuna anakayemuelekeza katika maamuzi yake.

Sumaye ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chadema, amesema, anakubaliana na Rais kuwa ana mamlaka ya kupanga watu wake na hakuna mtu anayeweza kumuingilia katika hilo lakini anatakiwa kutii hisia za wananchi wake.

“Nimemsikia Rais akisema kwamba yeye haambiwi, yeye ndio Rais, ni kweli, akasema alichukua fomu ya kugombea urais yeye peke yake kwa hiyo anatenda kazi zake anavyotaka, ni kweli lakini ni nani alimpigia kura? Ni watanzania ndiyo waliomfikisha pale,” amesema Sumaye.

Amesema, haki itendeke kwenye jambo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusishwa na tuhuma mbalimbali na kuwa limezungumziwa na rais, mawaziri na inaonekana mikanganyo ya dhahili na inaonekana pia kuna mtu anabebwa.

“Kama mkuu wa mkoa anafikia mahali anavamia kituo cha habari, waziri anayehusika na habari anakwenda anasikitika, lazima kuna tatizo, mimi Makonda nikisikia hata kesho ameingia mahali amepiga watu makofi wala sitashangaa, ametukana watumishi mbele ya kadamnasi sishangai, kwa sababu kama kweli yale yaliyoandikwa ni kweli, amefika mwisho wa uwezo wake,” amesema.

Makonda amekuwa katika kipindi kigumu cha kukabiliwa na tuhuma nzito za kumiliki vyeti vinavyotajwa kuwa vimetokana na jina la mtu mwingine aitwae Paul Christian, aliyefaulu mtihani wa taifa wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari ya Pamba, jijini Mwanza.

Isitoshe, Ijumaa ya wiki iliyopita, alijiongezea mzigo wa kashfa alipofuatana na polisi wenye silahausiku na kuvamia kituo cha habari cha Clouds Media, kilichopo Mikocheni, na kutaka kulazimisha kurushwa kipindi cha Shilawadu kwa namna atakavyo.
 
Attachments

  • VID-20170321-WA0085[1].mp4
    14.2 MB · Views: 59

Mmmmh yetu macho
 
Kelele zimezunguka nyumba ya makonda na babu yake,hatapata usingizi,na Dar ndio uwanja wa kila kitu,muda si muda ataanza kuzomewa.

Clouds wako karibu na asilimia 95 ya wasanii,

Huwezi kupambana na redio mbili kubwa kabisa jijini kama E FM na Clouds
 
Hivi hawa watu wanapatawapi KIBURI CHA KUWA NA UHALALI WA KUMNYOOSHEA KIDOLE MAGUFULI?????....hili hali wao ndio WACHAFU KUPINDUKIA.....
RAIS wetu komaa kuwanyoosha vizuri.......KIZURI NI KWAMBA YALE YOTE aliyo yaahidi AMBAYO YANA WAGUSA WANANCHI walio wengi,,NDIO MAANA HATUSIKII MIANO ya sisi mafukara,,RAIS yetu anayatekereza IPASAVYO.....hata kama kuna mapungufu ni MACHACHE maana hata yeye ni BINAADAMU......TUNACHOKIONA SASA NI KUBANA MASLAHI YA WALE MAJIZI AMBAO NI WACHACHE na ndio wapo mstari wa mbele kweli kupiga MIANO maana yamebananishwa kwenye ANGLE.........
 
Waliokaangwa wako wapi?
Shangaa mkuu na hicho kikaango kikowapi..hiyo ni sawa na kupiga mluzi ukiwa na uji mdomoni.tena wa moto...mzee magu na makonda na watanzania tuliokuwa tunataka mabadiliko ya ukweli na sio fitna na unafiki wa akina sumaye tuchapeni kazi.alikuwa wapi enzi zake kuiweka nchi vizuri...anahasira na mkwere anajua alivyofanywa mwaka 2005..kikwete mtoto wa mjini alimfanya huyu mzee wa watu kupoteza dira kama mjusi aliyedondoka toka darini...
 
Kumbe wewe ni mmoja wa wale wanaosapoti utapeli wa makonda? Uvamizi alioenda kuufanya pale clouds.
 
Mmmmh yetu macho
c946c9ae546504b85cc33af72b587988.jpg
.
 
Kama kuna maneno ambayo ninayakumbuka vyema kipindi cha Kampeni basi ni kauli ya Mhe.Fredrick Sumaye kuwa Ndani ya CCM hakuna wa kumshika shati Magufuli!!!
 
Kelele zimezunguka nyumba ya makonda na babu yake,hatapata usingizi,na Dar ndio uwanja wa kila kitu,muda si muda ataanza kuzomewa.

Clouds wako karibu na asilimia 95 ya wasanii,

Huwezi kupambana na redio mbili kubwa kabisa jijini kama E FM na Clouds
Hivi kwanini huwa mnapenda kutunga na kuishi kwa HISIA ambazo hata haziwezekani. HAO WASANII 95% Mbona HAWAJAWAPA POLE HAO CLOUDS Kwenye TUKIO LA UVAMIZI - WAKO KIMYA
 
David Rockefeller amekufa jana... alibadilishiwa moyo mara 7. sasa huyu anae jifananisha na Mungu wakati ana Moyo mmoja tena wenye matundu, anasahau kama kuna kifo, na awezi lipiza visasi kamwe. cheo ni dhama hata hapo ikulu huwez ishi zaidi mika mitano.
 
Ukitawala kwa kufuata hisia za watu hutafika mbali.

Kama Sumaye anaamini kuhusu kutawala kwa hisia basi hatuna wapinzani.
 
Back
Top Bottom