Sumaye ameitaka Afrika kutokomeza rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye ameitaka Afrika kutokomeza rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Sep 11, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amezitaka nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kupambana na makundi na kuwalipua wala rushwa na wapokeaji kwa kuwachukulia hatua.
  Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 20 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, (OUT).
  Katika mada yake iliyokuwa ikizungumzia kuhusu changamoto za kupunguza umaskini nchini, Sumaye alisema nchi za Afrika zipo nyuma kimaendeleo na kwamba yapo mambo mengi yanayotakiwa kufanyika.
  Alitaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni nchi kuwa na serikali inayopambana na makundi yote mabaya hasa rushwa.
  "Lazima tuipige vita rushwa ili kile kidogo kinachotakiwa kipatikane basi kipatikane kwa ajili ya huduma za wananchi na sio kupotea njia," alisema.
  Alitaka nchi zifanye biashara ambazo zitaweza kuzimudu na kutolea mfano Tanzania.
  "Tusiuze tu vitu kwa mfano magogo, pamba na madini nje ya nchi, tunatakiwa vitu hivi tuvibadilishe kuwa thamani ndio tuvipeleke nje kwenye soko la biashara, tunaiuzia magogo China halafu yeye anayabadilisha kuwa vitu vya thamani anakuja kutuuzia sisi tena, kwa nini sisi tusifanye vyote hivyo, tuwauzie wao," alisema.
  Kuhusu rushwa na utawala bora, Sumaye alisema lazima nchi ifikie mahali iwe na utaratibu wa kuhakikisha jambo hilo halivumiliki kwa sababu limekuwa likiigawa jamii katika kundi la wenye utajiri na maskini.
  Mtazamo wake kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa sasa inafanya kazi yake ipasavyo kutokana na kuanzishwa wakati akiwa madarakani, alisema anafikiri inafanya kazi yake.
  Kuhusu nini kifanyike, Sumaye alisema nchi inatakiwa kuwa na utawala bora ambao utawezesha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya watu wote.
  Pia alisema nchi inatakiwa kuhakikisha inakuwa na utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu na kuwepo na matumizi sahihi ya mali za taifa ili kila Mtanzania aweze kunufaika nazo.
  Naye, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette, alisema kuwa, katika maadhimisho hayo miadhara ya majadiliano iliyotolewa imelenga jamii na serikali kwa ujumla.
  Alisema lengo lake ni kutoa michango yao kwenye maeneo tofauti ambayo serikali imejiwekea katika kuyafikia maendeleo.
  Profesa Joseph Mbwiriza wa OUT akichangia majadiliano hayo, alisema suala la umaskini ni kubwa na watu wengi wapo nje ya mfumo rasmi wa uchumi.
  "Wanawake wengi hatuwatambui, kazi wanazozifanya haziingii kwenye takwimu zetu za kiuchumi za taifa, nini kifanyike tutekeleze Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) ili kazi zao na za wengine zitambuliwe kisheria, " alisema.
  Katika maadhimisho hayo mijadala mbalimbali ilitolewa ukiwemo uliokuwa ukiangalia kupotea kwa maadili kwenye jamii ya Tanzania.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! Naona anataka kucheza karata tena. Ila asante kwa ujumbe wako mzee kapumzike vyema na kiinua mgongo safi.
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Huyu ndiyo mwasisi wa mauaji tanzania ktk maandamano aliua watu pemba 2001 hana jipya anatafuta pa kutokea amebanwa na mary nagu kule Hanang
   
 4. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Alishindwa kumshauri Ben leo anawashauri marais wa bara zima? kazi kwelikweli
   
 5. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani lazima kila mtanzania awe Rais? Just curious..ok, tumekusoma Sumaye!
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mpaka tufike 2015 wataibuka wengi wa kuelezea udhaifu wa SSM yao ili mradi tu wanataka kiti kile!!! Wazee pumzikeni. Hii nchi ina wenyewe kwa sasa maana nyie kwa utawala wenu mlishindwa!!!
   
 7. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,312
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Rushwa ndani ya chama chake ccm imemshinda.leo anataka wenzake wakomeshe rushwa Afrika wapi na wapi?.
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  arudishe kwanza pesa aliyokwapua ppf mara baada ya kupata u pm!kinara wa rushwa huyu mzee
   
 9. A

  August JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hivi hakupata mashamba ya nafco kwa kupitia cheo chake? atoe kibanzi kwenye jicho lake kabla ya kuangalia kibanzi kwenye jicho la wengine
   
 10. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu jamaa mbona simwelewi kabisa. Kauli zake na matendo ni tofauti kabisa. Mbona wakati wa utawala wao yeye ndiye aliongoza kwa rushwa
   
 11. M

  Mkumbavana Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli nyani haoni kundule
   
Loading...