singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,538
Sumaye alipoingia Ukawa kwa gia ya ‘reverse'
TUKIO kubwa katika siasa za Tanzania wiki iliyopita ilikuwa ni lile la Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Frederick Sumaye kujiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga Ukawa, ingawa hakutaja anaelekea chama gani. Kujiunga kwa Lowassa Ukawa kunatokana na tetesi zilizosambaa awali za yeye kuhamia Chadema.
Kuhama kwa Sumaye CCM na kujiunga Ukawa, ni tukio lililofuata baada ya Waziri Mkuu mwingine wa zamani, Edward Lowassa kujiunga Ukawa (Chadema) na hatimaye kuteuliwa kuwa mgombea urais.
Hatua hiyo ya Sumaye inanyanyua siasa za Tanzania katika hatua nyingine moja ya juu zaidi. Ingekuwa ni Lowassa pekee ambaye kahamia upinzani tungesema, ‘aagh huyo mmoja tu?'
Sasa ni vigogo wawili. Woga miongoni mwa wananchi kuwa kuingia upinzani ni jambo la hatari na linaweza kukuharibia mambo yako hata ya binafsi utakuwa umepungua sana, kama sio kuondoka kabisa.
Kwa Sumaye kujiunga Ukawa kunatoa ishara kuwa CCM itabidi wafanye kazi ya ziada katika mikoa ya kaskazini ya Arusha na Kilimanjaro kuweza kupata walau viti vichache vya ubunge na kura za urais kwani Lowassa na Sumaye ni miongoni mwa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa katika eneo hilo.
Hata hivyo, hotuba ya Sumaye ya kujiunga na Ukawa ilishangaza wengi. Haikuwa aina ya hotuba tulizozizoea kutoka kwa wapinzani wengi ambao wamehama CCM. Kwangu binafsi, Sumaye alijaribu kadri alivyoweza kutokuwa mnafiki na kufuta imani yake juu ya uzuri wa CCM, kisa tu anahamia upinzani.
Sumaye hakuiponda CCM (na ningeshangaa kama angeiponda kama wapinzani asilia ambao wanaamini CCM na mtangulizi wake TANU hawajafanya chochote katika miaka zaidi ya 50 ya uwepo wake).
Hata hivyo, Sumaye alionesha kutoridhishwa na mchakato wa uteuzi akirudia madai yaliyowahi kutolewa Profesa Mark Mwandosya kuwa viongozi wa juu wa chama hicho tayari walikuwa na majina ambayo yangeunda tano bora. Sumaye pia alimsifu Dk. John Magufuli kuwa ni kiongozi mzuri na muadilfu aliyepita bila kutoa rushwa, ingawa ana upungufu wake wa kibinadamu.
Swali moja ambalo nimekuwa nikijiuliza, iwapo Lowassa angeshinda tiketi ya CCM, Sumaye angesemaje? Je, angethubutu kumsifu kuwa alipita bila kutoa rushwa? Nionavyo, jawabu ni hapana na ndio maana wachambuzi wengi walishangazwa na hatua ya Sumaye.
Kwa upande mwingine, Sumaye hakumsifu Lowassa katika mkutano wake wa kutangaza kujiunga Ukawa. Iwapo Sumaye angemsifu Lowassa ingekuwa maajabu makubwa, ingawa hata yeye kujiunga na muungano wa Ukawa ambao mgombea wake ni Lowassa pia yalikuwa ni maajabu ya aina yake. Hii ni kwa sababu ya historia iliyotokana na kinyang'anyiro cha kupigania nafasi ya ugombea wa CCM.
Wakati wa kinyang'anyiro hicho, Sumaye alinukuliwa akikitahadharisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuacha kuteua mgombea urais, ambaye anatumia fedha kuwahonga wananchi ili wamchague katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba na kwamba hatakubali kuona jina lake linakatwa kirahisi na akaendelea kuvumilia.
Baadhi ya wachambuzi wa siasa walitafsiri kauli hiyo kuwa ilimlenga Lowassa, jambo ambalo hata mtoto wa Mwalimu Nyerere, Makongoro alilitaja katika uzinduzi wa kampeni za CCM, Jangwani jijini Dar es Salaam, siku ya Jumapili.
Nukta nyingine muhimu katika hotuba ya Lowassa ni pale aliposema ameenda upinzani ili kuimarisha CCM na si kuidhoofisha na kwamba anaamini kwa yeye kuingia upinzani CCM itabidi wakaze buti ili kushinda. Lakini katika nukta nyingine iliyoleta mgongano na hiyo hapo juu, Sumaye alisema anahamia Ukawa kuwasaidia kuendesha serikali maana wengi kati wanasiasa walio huko hawajui kuongoza serikali.
Kauli hii kwa baadhi ya wachambuzi wanaiona kama kwanza ni dharau kwa viongozi wa upinzani na labda badala ya kujenga imani ya wananchi kwa upinzani inaweza kuondosha au kupunguza imani hiyo. Pili, kauli ya Sumaye inaleta picha kuwa sasa Ukawa kimsingi inaenda kuwa CCM – B.
Sumaye hakumung'unya maneno kuwaambia wananchi kuwa Ukawa bila msaada wa viongozi wa aina yake haitafanikiwa kuleta mabadiliko ya haraka yanayohitajika na wananchi. Kwa maneno yake mwenyewe alisema mabadiliko yatachukua muda mrefu sana.
CCM hawakusita kutumia kauli hii kuibomoa Ukawa kuwa ni muungano wa watu wasiojua kazi hadi kuhitaji kufundishwa na wachezaji wa mkopo kutoka CCM na kwamba huko ni kukiri udhaifu wa upinzani.
Kwa mtazamo wangu, baada ya kumsikiliza Sumaye, hitimisho langu ni kuwa ameingia Ukawa kwa ‘reverse gear' – kinyume nyume. Kauli zake zimeleta maswali mengi na labda hata kuipatia CCM silaha za kumuangamiza na kuiangamiza Ukawa.
Sumaye, katika nukta moja ya hotuba yake alitaja hata hoja za ukaskazini na kujijitetea kuwa hiyo sio sababu iliyomlepeleka yeye kuingia Ukawa. Kuitaja hoja hiyo hata kabla CCM hawajaiibua ni suala jingine lililoonesha Sumaye kaingia Ukawa kinyume nyume. Kwa namna Sumaye alivyoingia Ukawa, si ajabu basi CCM waliona fursa nyingi katiba hotuba yake za kuishambulia Ukawa na Sumaye. Hotuba ya Sumaye imeonesha wazi kuwa hazijui vema siasa za upinzani ambazo hazihitaji ukweli mtupu.
Je, Sumaye ata –‘fiti' katika siasa vyama vya upinzani. Ni muda pekee unaoweza kutupa jibu la swali hilo katika kipindi hiki muhimu cha kampeni.
Chanzo RaiaMwema
Toleo la 420
28 Aug 2015