Sumaye aiangukia Serikali wananchi kuvamia shamba lake la ekari 33 Mabwepande jijini Dar es salaam

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,491
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye,ameiangukia serikali na kuomba msaada baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia eneo lake la ekari 33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Serikali imemuahikikishia Mhe. Sumaye kuwa haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge wala tajiri hivyo itahakikiha inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki mbili kwa kua imesikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wananchi wa kitongoji cha Kimondo mtaa wa mji mpya Kata ya Mabwepande na Mhe.Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi, Mkuu waWilaya ya Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro huo ambao Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali kuingilia kati ni lazima busara kutumika. Alizitaka pande hizo mbili kuiachia serikali kwa wiki mbili ili kutafuta njia bora ya kumaliza tatizo hilo huku wananchi wakitakiwa kuache kuendelea na ujenzi na kugaiana maeneo katika shamba hilo.

“Serikali ya Rais Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa tayari kumsikiliza Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na kusikiliza wananchi ili kutenda haki tunatambua migogoro ya ardhi ilivyokuwa na athari kwa jamii hatuna mpango wa kumkandamiza tajiri wala mnyonge,”alisema. Alisema katika eneo hilo anajua jinsi wananchi walivyotumia nguvu katika kuwekeza ujenzi na rasilimali zao lakini kwa sasa wasitishe shughuli hizo na kuendelea kugawana maeneo na Sumaye pia kuacha uwekezaji ili kutafuta suluhu.

Zipo njia nyingi tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa kuangalia iwapo mzee wetu alikiuka taratibu kweli za kumiliki ardhi kama ilivyodaiwa na wananchi hatua gani serikali tuchukue,”alisema. Alisema pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali hasara kwa kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi hao ambao hawana makazi au Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei nafuu.

Alizitaka pande hizo mbili kutambua umuhimu wa kulinda amani katika mgogoro huo kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia nguvu.Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya utambuzi wa wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye. Awali katika mkutano huo Mhe. Sumaye alimueleza Mhe. Makonda jinsi serikali ilivyo na kazi ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia busara zake kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.

“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu sana hasa kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli eneo hili namiliki kihalali nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka na nilikuwa katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa kujenga Chuo Kikuu,”alisema. Alisema yeye na familia yake waliuziwa eneo hilo toka mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.

Diwani wa kata hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo lilikuwa pori na Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha uhalifu ikiwemo wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu mbalimbali. Alisema kutokana na hatua hiyo walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na ushirikiano kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha maji alikataa kuwapa wananchi .

Suzan alisema kutokana na hasira za wananchi hao kwa kukosa huduma za kijamii kwa muda mrefu ikiwemo eneo hilo kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo cha polisi waliamua kuvamia na kujigaia maeneo. Mmoja wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri kweli hawana umiliki halali wa eneo hilo na katika hatua ya kutafuta makazi walivamia msitu huo uliotelekezwa na Sumaye.

Alisema wanaamini kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora maeneo yaliyotelekezwa na wawekezaji watasaidiwa. WAKATI huo huo Makonda alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na mchanga, wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India Sules Waljan wanaochimba mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande. Hatua hiyo imekuja baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na alipowahoji wafanyakazi na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema hawana.

Makonda amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill ili kutoa maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama kubwa kwa uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika vyanzo vya maji na matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni makubwa.
 
Hili likimalizika litakuwa jambo la Maana la pili baada ya kutibiwa Muhimbili na hili la pili kufanywa na serikal tangu uhuru maana wakati wa kampeni alikuwa anasema hakuna hata jema moja limefanywa tangu uhuru!!
 
Huyo Sumaye peke yake ana miliki ekari 33 wakati huo huo wapo wananchi zaidi ya 500 wamejibana kwenye eneo la nusu ekari. Hii haijakaa sawa. Halafu Sumaye aendelezi shamba kwa namna yoyote ile...utetezi wake ni kwamba eti analipia kodi ya ardhi...Kodi ya ardhi ni suala moja na kuendeleza ardhi ni swala jingine.

Wananchi wapo sahihi kabisa kujichukulia maeneo kwenye shamba hilo. Na bado mashamba mengine ya Morogoro...huko nako kuna mashamba ya Sumaye na aliyapata wakati akiwa waziri mkuu maekari kwa maekari. Wananchi nayo wajibebe tu maana hakuna namna.
 
Hajaiangukia serikaliii...ila n wajibu wa serikali kutatua migogoro ya wananchi wake.. pindi inapojitokezaaaa.... na ni haki yake Sumaye kusikilizwa.
Hivi uwa unasikiliza vyombo vya habari? Ni watu wangapi hadi sasa tangu rais magufuli ameingia wamefutiwa hati zao za ardhi na maeneo hayo kupewa wananchi? Unadhani hilo litafanywa tofauti kwa Sumaye? Ndio maana tunasema Sumaye ameiangukia serikali ili imstili.
 
Kwa nini Hati yake ifutwe? While anapamiliki kihalali n miak 9 tuu je uandhani sheria imetamkaa uendelezaji wa eneeo n kwa njia zipi? .na unaushahidi kuwa hajawahi kupaendelezaa?
Watu wana maeneo makubwa tena n wawekezaji na hawajafanya kitu chochote ..
While yeye kanunua kwa shughuli zake binafsi..
 
Huyo Sumaye peke yake ana miliki ekari 33 wakati huo huo wapo wananchi zaidi ya 500 wamejibana kwenye eneo la nusu ekari. Hii haijakaa sawa. Halafu Sumaye aendelezi shamba kwa namna yoyote ile...utetezi wake ni kwamba eti analipia kodi ya ardhi...Kodi ya ardhi ni suala moja na kuendeleza ardhi ni swala jingine.

Wananchi wapo sahihi kabisa kujichukulia maeneo kwenye shamba hilo. Na bado mashamba mengine ya Morogoro...huko nako kuna mashamba ya Sumaye na aliyapata wakati akiwa waziri mkuu maekari kwa maekari. Wananchi nayo wajibebe tu maana hakuna namna.
Wananchi hawana haki ya kuvunja sheria... hakuna mtu yupo juu ya sheriaaa nenda mpanda hekar 100 zimepewa muwekezaji wala hajazigusaaaa. Tz kuna maeneo mengi yameporwa. Nenda arusha kuna falme za kiarabu.
Hiyo n chuk...acha chuki za kisisas mda wa kampen umeisha... kulipa visasi hakutasaidiaa...
Tunataka tufanye mambo kwa mujibu wa sheria. Na haki kila pande.
 
Sina nia ya kumwonea Sumaye inawezekana kabisa hilo eneo ni la kwake kihalali ila mabadiliko tuliyokua tunahubiri anaweza akatumia busara na kuwaachia wanachi hilo eneo wanaovamia maeneo hayo sio kwamba wana sehemu nyingine ila hawana hata pa kujenga,kama eneo limekaa tokea 1997 mpaka sasa hivi bila kuendelezwa sio sawa ,nakumbuka wakati fulani wananchi walimpa zawadi baba wa Taifa sina hakika ni zawadi gani ila yeye akahoji kwani yeye ni Tembo ?? Vitu hivyo wapelekewe wananchi
 
Sumaye ameonyesha in mzalendo wa kweli. Tumeona wangapi wenye maeneo yao halali wakitumia nguvu na ubabe kuwatoa wavamizi na serikali ijaishia kusema kuwa ni kweli wavamizi wamekosea?
Lakini yeye kamtafuta DC waende na wananchi wamekiri kuwa wamevamia kinyume cha sheria kwa sababu wana shida. Naamini wakituma maombi kiungwana kwake awakatie kipande chake cha ardhi Sumaye hawezi kukataa na baada ya hapo wataishi vyema kama majirani wema
Hapa ndio mtaona ishara ya kiongozi mahiri
 
Huwa simfagilii Sumaye lakini hii ni haki yake. Hivi wananchi hawa wanaweza kuvamia mashamba ya viongozi wengine waliopo CCM. Hao wananchi watafakari km ardhi ingekuwa yao wangeona sawa kuvamia? Manispaa ya Kinondoni iwape maeneo mengine watu na Sumaye aliendeleze eneo lile.
 
hayo maeneo lazima aliyachukua kibabe wakati akiwa waziri mkuu
ekari 33 atazifanyia nini amwogope mungu
 
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye,ameiangukia serikali na kuomba msaada baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia eneo lake la ekari 33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Serikali imemuahikikishia Mhe. Sumaye kuwa haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge wala tajiri hivyo itahakikiha inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki mbili kwa kua imesikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wananchi wa kitongoji cha Kimondo mtaa wa mji mpya Kata ya Mabwepande na Mhe.Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi, Mkuu waWilaya ya Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro huo ambao Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali kuingilia kati ni lazima busara kutumika. Alizitaka pande hizo mbili kuiachia serikali kwa wiki mbili ili kutafuta njia bora ya kumaliza tatizo hilo huku wananchi wakitakiwa kuache kuendelea na ujenzi na kugaiana maeneo katika shamba hilo.

“Serikali ya Rais Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa tayari kumsikiliza Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na kusikiliza wananchi ili kutenda haki tunatambua migogoro ya ardhi ilivyokuwa na athari kwa jamii hatuna mpango wa kumkandamiza tajiri wala mnyonge,”alisema. Alisema katika eneo hilo anajua jinsi wananchi walivyotumia nguvu katika kuwekeza ujenzi na rasilimali zao lakini kwa sasa wasitishe shughuli hizo na kuendelea kugawana maeneo na Sumaye pia kuacha uwekezaji ili kutafuta suluhu.

Zipo njia nyingi tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa kuangalia iwapo mzee wetu alikiuka taratibu kweli za kumiliki ardhi kama ilivyodaiwa na wananchi hatua gani serikali tuchukue,”alisema. Alisema pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali hasara kwa kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi hao ambao hawana makazi au Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei nafuu.

Alizitaka pande hizo mbili kutambua umuhimu wa kulinda amani katika mgogoro huo kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia nguvu.Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya utambuzi wa wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye. Awali katika mkutano huo Mhe. Sumaye alimueleza Mhe. Makonda jinsi serikali ilivyo na kazi ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia busara zake kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.

“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu sana hasa kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli eneo hili namiliki kihalali nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka na nilikuwa katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa kujenga Chuo Kikuu,”alisema. Alisema yeye na familia yake waliuziwa eneo hilo toka mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.

Diwani wa kata hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo lilikuwa pori na Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha uhalifu ikiwemo wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu mbalimbali. Alisema kutokana na hatua hiyo walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na ushirikiano kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha maji alikataa kuwapa wananchi .

Suzan alisema kutokana na hasira za wananchi hao kwa kukosa huduma za kijamii kwa muda mrefu ikiwemo eneo hilo kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo cha polisi waliamua kuvamia na kujigaia maeneo. Mmoja wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri kweli hawana umiliki halali wa eneo hilo na katika hatua ya kutafuta makazi walivamia msitu huo uliotelekezwa na Sumaye.

Alisema wanaamini kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora maeneo yaliyotelekezwa na wawekezaji watasaidiwa. WAKATI huo huo Makonda alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na mchanga, wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India Sules Waljan wanaochimba mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande. Hatua hiyo imekuja baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na alipowahoji wafanyakazi na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema hawana.

Makonda amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill ili kutoa maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama kubwa kwa uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika vyanzo vya maji na matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni makubwa.
Chadema walimpa umeneja kampeni huyu jamaa! Mbowe akili zake bwana ha ha ha. Unajenga chama miaka ishirini,unaimba ufisadi miaka 20 dakika za mwisho unakuja wapa mafisadi hao hao waendeshe chama! Insanity
 
Hili likimalizika litakuwa jambo la Maana la pili baada ya kutibiwa Muhimbili na hili la pili kufanywa na serikal tangu uhuru maana wakati wa kampeni alikuwa anasema hakuna hata jema moja limefanywa tangu uhuru!!
Zilikuwa polojo kwa Nyumbu
 
Huyo Sumaye peke yake ana miliki ekari 33 wakati huo huo wapo wananchi zaidi ya 500 wamejibana kwenye eneo la nusu ekari. Hii haijakaa sawa. Halafu Sumaye aendelezi shamba kwa namna yoyote ile...utetezi wake ni kwamba eti analipia kodi ya ardhi...Kodi ya ardhi ni suala moja na kuendeleza ardhi ni swala jingine.

Wananchi wapo sahihi kabisa kujichukulia maeneo kwenye shamba hilo. Na bado mashamba mengine ya Morogoro...huko nako kuna mashamba ya Sumaye na aliyapata wakati akiwa waziri mkuu maekari kwa maekari. Wananchi nayo wajibebe tu maana hakuna namna.
Nikupokonywa tu
Huyu wanamchelewesha
 
Hivi uwa unasikiliza vyombo vya habari? Ni watu wangapi hadi sasa tangu rais magufuli ameingia wamefutiwa hati zao za ardhi na maeneo hayo kupewa wananchi? Unadhani hilo litafanywa tofauti kwa Sumaye? Ndio maana tunasema Sumaye ameiangukia serikali ili imstili.
Anatetea upande wake
Ila ukweli Ni Sumaye Ameipigia goti Serikali
 
Chadema walimpa umeneja kampeni huyu jamaa! Mbowe akili zake bwana ha ha ha. Unajenga chama miaka ishirini,unaimba ufisadi miaka 20 dakika za mwisho unakuja wapa mafisadi hao hao waendeshe chama! Insanity
Tushatoka huko kwenye kampeni
 
Duuh! Kweli huu ni ubepar hekta 33 kamik bila ata ya kuziendeleza? Wakat wananch wanahangaika na virobo eka
 
Back
Top Bottom