Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye (pichani), amefunguka kuhusu uamuzi wa Umoja wa Vijana wa CCM makao makuu kusitisha shughuli za kumsimika kuwa Kamanda wa Vijana wa Wilaya ya Hanang.
Akizungumza na maelfu ya wakazi wa mji wa Katesh juzi, alisema ni mawazo potofu kufikiri kwamba anahitaji ukamanda ili azunguke popote na hasa katika wilaya hiyo.
Mkutano huo ulitanguliwa na maandamano ya wananchi huku wengine wakiwa kwenye pikipiki na magari na pamoja na vikundi vya ngoma huku wengine wakiwa wamejipanga barabarani.
Maandamano hayo yalianzia nyumbani kwake Endasak hadi viwanja vya mkutano vilivyopo jirani na kituo cha mabasi.
Alisema jambo hilo halimshangazi kwa sababu alishapewa habari kuwa baadhi ya vijana hao walioandaliwa walikuwa wakisema hataapishwa mpaka baada ya uchaguzi mkuu upite.
"Nikajiuliza uhusiano ni nini kati ya ukamanda na uchaguzi mkuu. "Nimedokezwa na hii ingekuwa hisia ya mtu ye yote kuwa ati mimi nitatumia nafasi hiyo ya ukamanda kuzunguka wilayani kupinga mtu fulani au watu fulani wasichaguliwe," alisema bila kumtaja.
Alisema msimamo wake ni kutogombea ubunge wa jimbo hilo, ambalo kwa sasa linashikiliwa na Dk. Mary Nagu (CCM). Alisema anao vijana wengi tena wasomi katika jimbo hilo ambao anawaachia wagombee nafasi ya ubunge badala ya yeye katika umri mkubwa wa miaka 60 aliyonayo kung'ang'ania kugombea. "Nimekuwa mbunge wa jimbo hili kwa miaka 20 mfululizo, sasa hivi kuna vijana wengi tena wasomi wanaweza kugombea.
Siwezi kugombea ubunge, ninyi mnajua mimi nataka kugombea nini, au kuna mmoja hajui hilo?" Alisema yeye mpaka sasa anashikilia rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza aliyekuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo na ametoka madarakani akiwa hana kashfa. "Mnajua misingi ambayo nimekuwa ninasimamia na ninaendelea kuisimamia hadi leo.
Nimekuwa napigania maendeleo, umoja, upendo na amani. "Ni mpambanaji dhidi ya dhuluma, kugawa jamii kwa misingi ya ukabila au siasa na sina simile na rushwa, ufisadi na maovu mengine katika jamii," alisema.
Alisema alishangaa kupata taarifa kuwa UVCCM makao makuu Dar es Salaam wametoa taarifa ya kusitisha shughuli ya kumwapisha kwa maelezo kuwa kuna malalamiko hadi hapo baadaye wakati ilishatangazwa na UVCCM wilaya ya Hanang'.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda, alipoulizwa jana kuhusiana na kusitisha kumwapisha Sumaye, alisema alikuwa katika mkutano wa vijana jijini Arusha na kuahidi kuzungumza baadaye.