SUMATRA yawataka madereva kufika mwisho wa vituo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,858
Madereva wa daladala wametakiwa kufika katika vituo vyao vya mwisho kama ilivyoanishwa kwenye leseni zao ili kuwaepushia abiria usumbufu wa kuwakatishia ruti kwani kwa kufanya ni usumbufu wa hali ya juu kwa abiria husuika.
foleni%2Bpix.jpg

Akizungumza katika kipindi cha SUPAMIX kinachorushwa na E A Radio Meneja Leseni wa Sumatra Bwana Leo Ngowi amesema tayari wameshakamata baadhi ya madereva na kesi zao zipo katika hatua ya kuwafikisha mahakamani lengo likiwa kukomesha tabia hiyo.

Madereva mbalimbali wamekuwa na tabia ya kukatiza ruti za barabara zao kutokana na sababu mbalimbali na kupelekea usumbufu kwa abiria.

Baadhi ya madereva wamesema kwamba ubovu wa miondombinu katika ruti zao imekuwa chanzo kikubwa cha kukatiza pia upatikanaji wa abiria kwa baadhi ya maeneo hasa nyakati za mchana.

Chanzo: EATV
 
Back
Top Bottom