Sumatra: Hatuhitaji mrithi wa Majembe

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
Send to a friend

Hamad Amour

BAADA ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kuvunja mkataba na Kampuni ya Udalali ya Majembe Auction Mart, imesema shughuli zote za ukaguzi wa magari na leseni watazifanya wenyewe kwa kushirikiana na polisi. Mkataba huo ulivunjwa baada ya Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, kutaka Sumatra kusitisha mkataba wake na Majembe ifikapo Desemba 31, Mwaka jana.

Kisheria mkataba huo ulitakiwa kumalizika Januari 31, mwaka huu. Agizo la waziri lilifuatia malalamiko ya wamiliki wa Mabasi ya Abiria yaendayo mikoani (Taboa) na Umoja wa Wasafirishaji Abria Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa).

Taboa na Darcoboa walilalamikia Majembe kwamba imekuwa na mpango wa kujipatia kipato kwa kuwatoza faini kubwa zisizoendana na makosa husika. Afisa Uhusiano wa Sumatra, David Mziray, alisema kuanzia juzi mkataba wao na Majembe umevunjika hivi sasa kampuni hiyo haitakiwi tena kuwapo barabarani kwa niaba ya Sumatra.

“Kwa sasa Kampuni ya Majembe haitakuwepo barabarani tena, kwani mkataba wao na Sumatra umemalizika,” alisema Mziray. Mziray alisema hivi sasa shughuli zote za usimamizi na ukaguzi wa gari utafanywa na Sumatra wenyewe wakishirikiana na polisi kitengo cha usalama barabarani, sio mtu mwingine.

Pia, alisema Sumatra haina mpango wa kutafuta kampuni nyingine kuendesha shughuli zilizokuwa zikifanywa na Majembe na kwamba, hata ukiwepo hawezi kulitolea kauli kwa sasa.

“Naomba nisisitize kauli yangu nililiyotoa kwa leo ambayo natakiwa kunukuliwa,ni kuwa Majembe hawapo tena barabarani na usimamizi unaendeshwa na Sumatra ikishirikiana na polisi kitengo cha usalama barabarani,” alisema Mziray.

Aliongezea kuwa iwapo Sumatra itaona ipo haja ya kutafuta kampuni nyingine ya kufanya nao kazi, itafanya hivyo na kila kitu kitawekwa wazi ili wanachi wajue kitakachokuwa kinaendelea. “Iwapo tutafikiria kufanya maamuzi megine yoyote zaidi ya haya, basi tutawaalika (waandishi wa habari) mshuhudie kitakachokuwa kinaendelea,” alisema Mziray.

SOSI: MWANANCHI

WAZO: JE HATA TRA NAO WATAACHA KUWATUMIA MAJEMBE?
 
Back
Top Bottom