SUMATRA Dar mko wapi mbona daladala wanajipangia bei ovyo route ni moja lakini kila daladal lina nauli yake?

dutch2

JF-Expert Member
Sep 20, 2017
1,009
972
It's real boaring kwa SUMATRA wa Dar yani daladali zinajipangia nauli tu ovyo ovyo na wako kimya mfano mdogo ni;

Makumbusho Gongolamboto.
Gongolamboto Mawasiliano
Gongolamboto Kariakoo
Gongolamboto Tandika

Hizi route nimeziexperience wanajipangia nauli tupeni mwelekezo nauli ni shs ngapi au mtuletee mwendokasi nauli iwe standard.
 
it's real boaring kwa SUMATRA wa Dar yani daladal zinajipangia nauli tu ovyo ovyo na wako kimya mfano mdogo ni makumbusho gongolamboto
gongolamboto mawasiliano
gongolamboto kariakoo
gongolamboto tandika
izi route nimeziexperience wanajipangia nauli tupeni mwelekezo nauli ni shs ngapi
au mtuletee mwendokasi nauli iwe standard

Hii haihitaji SUMATRA.

Panda gari lipa nauli inayohitajika alafu subiri tuone atakupeleka wapi.
 
Nauli huwa imeandikwa karibu na mlango wa kuingilia mbele, ni sheria ya Sumatra.
 
Usisubiri sumatra, kama mnajua nauli halali goma kulipa na tafuta namba za sumatra uwapigie kuwapa taarifa ya hilo daladala. Ni muhimu kutizama risit unayopewa imeandikwa kiasi gani
 
Nauli huwa imeandikwa karibu na mlango wa kuingilia mbele, ni sheria ya Sumatra.
Mkuu hiyo hawaifuati

Mfano route ya Ubungo-Mbezi ni 400 lakini wanatoza 500, ukiwapa 400 wanaanza kuleta zogo
 
Hii haihitaji SUMATRA.

Panda gari lipa nauli inayohitajika alafu subiri tuone atakupeleka wapi.
issue inakuja pale unapotoa hela yakurudishiwa change ndo unajua nauli imepanda
 
Nauli huwa imeandikwa karibu na mlango wa kuingilia mbele, ni sheria ya Sumatra.
kwa nini route zote nauli isiwe standard at list mngekuwa na mambo ya premier class na economy class
mfano
posta makumbusho 400 T167
posta makumbusho 450 T122
posta makumbusho 500 T627 wote wanatumia barabara moja au SUMATRA wana 10% uku bora serikali ikabidhi tajiri mmoja au group la wafanya biashara waendeshe kama ulaya wanavyofanya hawa individuals hawaishi matatizo
 
Mkuu hiyo hawaifuati

Mfano route ya Ubungo-Mbezi ni 400 lakini wanatoza 500, ukiwapa 400 wanaanza kuleta zogo
kwa hiyo we unaogopa zogo, mtu mzima unakuaje muoga. lipa nauli kulingana na ilivyoandikwa kwenye ticket,ubavuni mwa gari na iwe sahihi kulingana na nauli walizopangiwa na sumatra mkoa
 
ngoja niwape maelezo kulingana na uzoefu wangu wa route ya gongolamboto -k/koo na ubungo/mawasiliano.

GONGOLAMBOTO TO K/KOO nauli ni sh.450/=
lakini mara nyingi chenji ya shilingi 50/= huwa inasumbua konda anaweza kukuomba kuwa hana hamsini kistaarabu unamuachia ila sio kwamba konda atalazimisha. mara nyingi watu hukatwa sh 500/= kutokana na ukosefu wa chenji ila kama una 450/= mpe hiyohiyo au toa mia tano halafu mwambie akurudishie 50/= yako akikataa hapo ndo patamu unamuanzishia vagi tu mpaka akupe 50/= yako

GONGOLAMBOTO TO UBUNGO/MAWASILIANO.
daladala hizi hupita njia mbili tofauti yaani
1.kuna zinatotoka gongolamboto hadi ubungo/mawasiliano via buguruni nauli 500
2.kuna zinatoka gongolamboto hadi ubungo/mawasiliano via t/segerea nauli 600

muhimu kabla hujapanda daladala jiridhishe kwanza na nauli iliyoandikwa ubavuni mwa gari sio kukimbilia siti utadhani utazikwa nayo.
 
Mkuu kuna wengine wanazingua sana.

Kuna route ya K/koo-Tegeta kupitia Ally Hasani Mwinyi road, then Bagamoyo road nauli ni 600.

Lakini kwa hiyo route ukiwa unashuka Kawe ni 400.

Wao wanataka ulipe 600 hata kama unashuka Kawe jambo ambalo linasumbua sana.

Mimi binafsi nimekorofishana nao mara kibao nikiwa nawapa 500 hadi Kawe lakini wao wanasema ni 600 ambayo ni hadi Tegeta
 
Back
Top Bottom