SUMATRA acheni kulala

SUMATRA acheni kulala

kande kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2011
Posts
234
Reaction score
89
Sumatra,

Ni sahihi wananchi walio ndani ya Jiji (hardly 10 Kilometres) kulipa nauli ya shilingi 1000/=? Hivyo ndivyo tunavyokamuliwa wananchi tunaoishi Buza Kanisani na kufanya kazi au biashara maeneo ya kuanzia Airport kwenda Gongolamboto.

Ni hivi, ninapaswa kulipa shilingi 400/= kwa bajaji inayotembea umbali wa Km 4 kutoka Buza Kanisani hadi Lumo mwisho wa Rami. Kutokea hapo Km 4 zingine mpaka Jet (Nyerere Road) nalipa sh 300/= Kutoka Jet mpaka mfano Airport Km 2, nalipa 300/= nyingine na tayari sh 1000/= inakuwa imeenda zake ndani ya km 10. Kurudi nyumbani, sh 1000/= nyingine inaenda zake.Wakati huo mtu anayetoka Tandika mpaka Msasani au Gongolamboto mpaka Msasani analipa ikizidi sana sh 700/=. Usawa uko wapi? Kwa nini hamfanyi research ya route mpya kwa minajili ya kurahisisha usafiri na kupunguza makali ya maisha kwa wananchi? Lakini pia kwa nini hakuna route ndefu mfano ya Buza Kanisani - Kariakoo na badala yake lazima tukapande gari jingine Tandika ndo tufike Kariakoo? Wakati mmetoa route ya Tegeta - Kariakoo japo kuna Kariakoo - Mwenge?

Pendekezo langu ni kuwa muanzishe route mpya ya Gongolamboto - Tandika via JET kwa kuwa sasa junction ya JET imekamilika. Mbali ya kuondoa usumbufu na kupunguza ukali wa maisha, lakini pia mtapunguza msongamano Nyerere Rd na Mandela Rd japo kidogo. Hili ni sambamba na kuanzisha route ndefu ya Buza Kanisani - Kariakoo.

Amkeni bwana, usingizi wenu unatuumiza!

Wakatabahu.
 
Back
Top Bottom