Sukari v/s Bunge la Budget: Sawa na kuzuka kwa Kikombe cha Loliondo

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,314
72,740
Bunge la budget lineanza takribani wiki mbili zilizopita, hapo ndipo unajadiliwa mwenendo wa bajeti kwa nchi ndani ya mwaka ujao na kuna mpango wa maendeleo wa miaka mitano. Ni bajeti ya muhimu hasa ikizingatiwa kuwa ni ya kwanza kwa rais mpya.

Lakini bajeti inaanza kushika kasi na kwa habari tunazosikia bungeni kunaanza kupanba moto ghafla drama zinaanza. Sukari,sukari. Kila mtu amehamishwa mawazo kwenda kwenye sukari, imekuwa ndio agenda ya Taifa kila mtu anazungumzia hilo wakati kuna wizara ya biashara, ya kilimo, Bodi ya sukari, TRA nk. Wote wameshindwa mpaka Rais ndio awe mtekelezaji?Au hizi ni mbinu za kututoa akili kwenye Budget na ikishapita basi na sukari inakuwa IPO ya kutosha?

Hii trick ni kama ile ya miaka ile ambapo upinzani ulianzisha maandamano yasiyo na ukomo ikazuka dawa ya magonjwa yote "kikombe cha babu Loliondo" na watanzania wote wakasahau yote na kugeukia Loliondo. Je hili la sukari laweza kuwa limezalishwa kama lile la Loliondo kwa malengo yaleyale ya kupoteza lengo?
 
Hata hao viongozi wanaolivalia njuga na kuvamia magodown ambayo ni kawaida kuhifadhi bidhaa hiyo ni wa aina ya Makonda, wale wazoefu wanaonyesha kujua kuwa hii ni fix
 
Back
Top Bottom