SUKARI NYEUPE.

SUKARI NYEUPE.

Kaie

Member
Joined
Oct 9, 2016
Posts
48
Reaction score
24
Hii ni aina ya sukari iliyosafishwa sana,ambapo huwa na madhara inapotumika kwa kiwango kikubwa.
Sukari inaposafishwa,madini&vitamini huondolewa,na kubakiza kalori tupu tu. Lakn mwili hauwezi kutumia kama ilivyo,inahitajk vitamini ili ifae kutumika mwilini. Kwahiyo mwili unachukua vitamini hivyo kutoka ktk vyakula vingine vya asili sababu ambayo hupelekea upungufu wa vitamini.

Magonjwa mengi yanaweza kutokana na matumizi makubwa ya sukari hii iliyosafishwa sana,magonjwa ambayo ni mapya hapa Afrika, kama vile kiwango cha chini cha sukari mwilini,kisukari, umagonjwa ya moyo,unene na upungufu wa vitamini, madhara mengine ambayo hutokana na matumizi makubwa ya sukari nyeupe ni kama vile, kuwa na wasiwasi,hasira, na kukosa umakini ktk masomo hata kazini pia. Hata tabia ya uhalifu wa kipumbavu imegunduliwa kusababishwa na athari za matumizi makubwa ya sukari.

Kuoza meno huongezska popote matumizi ya sukari inapozidi, ktk nchi nyingi Afrika kuna madaktari wa meno wachache sana,kwa kadri ulaji wa sukari unavyopanda kutokana na matumizi ya pipi,Ice cream, soda, na keki(maana humo ndimo sukari nyeupe inapatikana) jaribu kufikiri taabu itakayotokea wakati meno ya waafrika yaliyo na afya yanapoanza kuoza!

Bakteria walio kinywani huyeyusha sukari iliyo kwenye meno na kuzalisha asidi za latic,formic&asetiki, asidi hizi hushambulia gamba la jino kisha kusababisha matundu kutokea.
Meno ni muhimu sana lakini hupotezwa kwa mfumo huo.

USHAURI
Basi mlapo au mnywapo au mtendapo neno lolote fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
1Kor 10:31.

UJUMBE
Siyo kila chenye ladha ya utamu kinafaa kuingizwa mwilini vingine ni uchafu na sumu kuweza kuangamiza uhai wako.
CHUKUA HATUA.
 
Back
Top Bottom