Sugu moto chini: CCM tunawambia haya ili mje muwe wapinzani makini

Kwa mara ya kwanza nimejua jimbo la mbeya mjini walichagua jembe lenye makali. Anashangaa twiga warefu kuliko ndege kusafirishwa kwa mdege kwenda ulaya....
 
Kinacho takiwa kung'oka ni nyumba nzima wala siyo mabati pekee.Nasema hivyo nikimaanisha kwamba mawaziri wapya hawato kuwa tofauti kiutendaji na hawa.JK atatumia vigezo vile vile ambavyo vime prove failure.Tatizo kubwa ni magogoni.Ang'olewe yeye pia.
 
Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Joseph Mbilinyi, amesema Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete wanaotamba kuwa hawatang'oka kwenye wadhifa huo, watang'olewa kwa kimbunga kinachokuja.

Akizungunza Mbunge Mjini Dodoma saa 6:45 mchana leo, amemhakikishia Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kuwa moto uliowashwa na wabunge bila kujali itikadi zao kisiasa, lazima mawaziri waliotajwa kuhusika katika kashifa ya ubadhirifu watangoka.

Amesema hata kama kimbunga hicho hakitang'oa nyumba nzima,lakini kitaondoka na paa la nyumba hiyo, akimwaanisha kuwa iwapo mawaziri hao wataendelea kung'ang'ania nyadhifa hizo, Waziri Mkuu Pinda atang'olewa kwa upepo huo.

"Sitanii, huu ni upepo wa kimbunga, kama hautang'oa nyumba, utaondoka na paa la nyumba, inasemekana kuna tetesi kuwa wameambia huu ni upepo tu utapita, nakuhakikishia Mheshimiwa Spika, upepo huu wa kimbunga lazima utawang'oa, watake wasitake", amesisitiza Mbilinyi.

Amewataka ni vyema mawaziri walioshindwa kazi ya kuwajibika waachie ngazi, kama walivyoombwa na Mbunge wa Vunjo, Bw. Agustine Mrema wa TLP. Mrema aliwaambia mawaziri hao kuwa iwapo kazi ya kuwajibika imewashinda, ni bora wakae kando ili wengine wafanye kazi hiyo.

Huku Waziri Mkuu Pinda akionesha kutabasamu, Bw. Mbilinyi amesema Tanzania ni moja ya nchi zenye vivutio vya kila aina, wanyama wanachukuliwa na kusafirishwa kinyemela bila kufuata taratibu za nchi, na kwamba baadhi ya wawekezaji huingia nchini na wageni kwa mgongo wa Luteni Kanali Mstaafu Abdulhaman Kinana.

Amesema kazi yao kama vyama vya upinzani Bungeni ni kupambana na Chama Tawala, ili kijisahihishe kwa wananchi, huku akiwataka wafanye maandalizi ya kushindana na CHADEMA watakapokuwa wapinzani.

"Mheshimiwa Spika, kazi ya kambi ya upinzania Bungeni ni kukosoa kila uozo unaofanywa na Chama Tawala, waache kufanya madudu, hii itawasaidia watakapokuwa wapinzani nao wajipange kutukosoa tutakapoingia madarakani kuwatumikia watanzania", anasema.

Akishangiliwa na wabunge, huku wengine wakivunjika mbavu kwa vicheko, Bw. Mbilinyi, amesema upepo huo wa kimbunga, hautapita hivi hivi lazima utaharibu nyumba, kama itashindikana basi paa la nyumba hiyo litang'oka na waliomo watahama.
 
Kikwete naona kaziba masikio anajifanya hasikii kinacho endelea
 
Du inaonekana huko CDM kama ni timu basi ni mithili ya Barcelona, kwani kila anayesimama kazi yake ni ya kusisimua. Wengine walikuwa wanabeza oooh Sugu hamna kitu sasa inaonekana kumbe naye jemebe la uhakika, kazi buti Sugu hadi kitaeleweka tu
 
Imagine bunge bila CDM. Imagine ile miaka ya ndiyoooooooo. Imagine ile miaka ya kulala na kulambo posho bwerere. Imagine miaka kadhaa ijayo wakati CDM imeshika dola.

Nchi hii imeliwa sana na viwavi ccm lakini pamoja na kuchelewa huku bado ni sahihi kurekebisha mambo. Asante sana makamanda. Big up Hon. Mbilinyi
 
Cloudz ya wafu fm ,watairusha kweli hii!

Hawawezi ila nina hakika wanamkubali, Sugu ni moja ya watu ambao hujifunza na kubadilika haraka!!

Unategemea nini toka vijana wakaao karibu kabisa na majembe kama Slaa, Zitto & Co!!
 
wananchi wanamzuka sana na juu yenu, kama tungekuja na mzuka huo walio nao wananchi nafikiri tungeng'oa hivi viti na kuwa piga navyo.
 
Mh. Sugu anaonyesha ni kwa kiasi gani watu wa mbeya hawakukosea kumpa usukani wa kuongoza jahazi lao. Na hii ni fundisho kwa majimbo ambayo bado yanakumbatia CCM.kwenye kutetea haki hakuna kuogopa!big up CDM
 
Mh. Sugu anaonyesha ni kwa kiasi gani watu wa mbeya hawakukosea kumpa usukani wa kuongoza jahazi lao. Na hii ni fundisho kwa majimbo ambayo bado yanakumbatia CCM.kwenye kutetea haki hakuna kuogopa!big up CDM

Kwa tunaomfahamu sugu hatujashangaa...harakati hajaanza leo
 
Safi sana kama CCM wanafikiri huu ni upepo basi wamepotea, hiki ni kimbunga na kazi ya kimbunga ni kuezua paa ama kuvunja nyumba nzima,wamekwisha.
 
magamba wametuona watanzania wapole sasa wanataka kutushika masaburi nakutuingiza vidole makalioni nawambia ccm walivyo wajinga wanajua mambo yataisha tu na ajiuzulu mtu lakini kwa hili tutaitisha maandamano ya tahalili square mngese.. au ya bengazi na bengazi tutakutana mnazi mmoja.
 
pinda alisema leo ndo tutajua huo mwafaka wa mawaziri wanaotakiwa kujiuzulu. Sasa sijui anasubiri nini kutuambia kama jk kamwambia ni upepo na yeye hajaridhika basi ni vyema ajiuzulu yeye ili amwache yeye na huo upepo utakaopita
 
pinda alisema leo ndo tutajua huo mwafaka wa mawaziri wanaotakiwa kujiuzulu. Sasa sijui anasubiri nini kutuambia kama jk kamwambia ni upepo na yeye hajaridhika basi ni vyema ajiuzulu yeye ili amwache yeye na huo upepo utakaopita

Usitegemee lolote kutoka kwa Pinda,labda kama umemiss kuona mzee mzima analia.
 
Back
Top Bottom