Sugu ataka tume kuchunguza vurugu za machinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sugu ataka tume kuchunguza vurugu za machinga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, May 11, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]
  [​IMG]
  MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu ameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuunda tume huru kuchunguza chanzo cha vurugu za wamachinga zilizotokea Novemba 4, mwaka jana jijini Mbeya.  Sugu alieleza hayo juzi alipomtembelea mmoja wa majeruhi wa vurugu hizo, Moses Mwakalukwa, mkazi wa Soweto jijini hapa ambaye anaendelea kuuguza mguu wake baada ya kujeruhiwa na polisi kwa kupigwa risasi.  Alisema kuwa baadhi ya wananchi bado wana machungu yaliyotokana na vurugu hizo, hivyo kama serikali haitawatendea haki kwa kuchunguza kwa kina na kuwachukulia hatua watu waliosababisha vurugu hizo, kuna hatari ya tukio hilo kujirudia katika siku za usoni.  Katika ziara hiyo Sugu alitoa kiasi cha shilingi 250,000 kwa ajili ya kumsaidia majeruhi huyo kwenda kupata matibabu hospitalini, ambapo awali Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) walimchangia kiasi cha shilingi 260,000 kwa ajili ya matibabu.  Akitoa shukrani zake kwa Mbunge, Mwakalukwa alisema kiasi hicho cha fedha kitamsaidia kwenda katika Hospitali ya Peramiho iliyoko mkoani Ruvuma kupata matibabu zaidi ya mguu wake.  Mwakalukwa alisema baada ya kupigwa risasi kwenye vurugu za Mwanjelwa, alilazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, ambako yeye na majeruhi wenzake walitembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na kuahidiwa kuwa serikali itawasaidia gharama za matibabu.  Hata hivyo alisema licha ya mkuu wa mkoa kutoa ahadi hiyo, hakuna msaada wowote alioupata kutoka serikalini hadi sasa na amekuwa akijigharimia mwenyewe, hali iliyomuathiri kimaisha yeye na familia yake.  Hata hivyo Kandoro alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, alikana kutoa ahadi hiyo na kusema kuwa wakati tukio hilo linatokea yeye alikuwa ni mgeni na hakumbuki kama aliahidi kutoa msaada wa aina hiyo.  Aidha, Kandoro alishauri kuwa kama kijana huyo anataka msaada wa serikali kutokana na tukio lililompata, anaweza kuandika barua na kuipeleka ofisini kwake akiomba msaada na iwapo serikali itajiridhisha kwa ushahidi kuwa alikuwa mhathirika.


  CHANZO : Tanzania Daima.

  chademablog.blogspot.com

   
Loading...