Sudan Kusini: Watu 50 wauawa Juba kufuatia mzozo wa mifugo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,236
2,000
Watu 50 wameuawa katika mzozo wa kugombea mifugo katika jimbo la Jonglei, Sudan Kusini, miongoni mwao wakiwemo watoto saba. Wizi wa mifugo umekuwa ukifanyika kwa karne kadhaa Sudan Kusini.

17323698_303.jpg


Watu 50 wameuawa katika mzozo wa kugombea mifugo katika jimbo la Jonglei, Sudan Kusini, miongoni mwao wakiwemo watoto saba. Waziri wa habari wa jimbo hilo, Akech Dengdit amesema wanawake 23 na wanaume 10 pia waliuawa jana asubuhi katika kile alichosema ni shambulizi la pamoja lililosababishwa na wezi wa mifugo na waasi wanaomtii Riek Machar.

Ameitaka serikali kuu ya Sudan Kusini kupeleka jeshi na polisi katika maeneo ya ndani kwenye jimbo la Jonglei ili kuimarisha usalama na kupambana na ghasia na wizi wa mifugo.

Wizi wa mifugo umekuwa ukifanyika kwa karne kadhaa Sudan Kusini na mara nyingine watoto wanatekwa nyara wakati wa wizi huo ili wafanye kazi za utumwa majumbani. Nchi hiyo pia iko katikati ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo maelfu ya watu wameuawa tangu mwaka 2013 baada ya kutokea mpasuko kati ya Rais Salva Kiir na Machar, aliyekuwa makamu wa rais.Chanzo: DW

Sudan Kusini: Watu 50 wauawa Juba kufuatia mzozo wa mifugo | Matukio ya Afrika | DW | 29.11.2017
 

popoma

JF-Expert Member
May 5, 2017
2,380
2,000
Tatizo hapa nchini tunachelewa kuna umuhimu wa kushikishana adabu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom