Sudan Kusini: Riek Machar ataka kwenda Juba na silaha zake

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,859
Kiongozi wa Waasi na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Kusini,Riek Machar amesema kuwa yuko tayari kurudi Juba akiwa na silaha na wanajeshi wake. Hayo yanakuwa masharti yake ya kurejea Juba.

Machar anapaswa kurejea Juba katika utekelezaji wa Mkataba wa Amani kati yake na Rais Salva Kiir. Machar akirejea Juba atarejeshewa nafasi yake ya Makamu wa Rais wa Sudan Kusini.

===================
Makubaliano ya amani nchini Sudan Kusini yapo hatarini baada ya kiongozi wa waasi Riek Machar kushindwa kurudi katika mji mkuu wa Juba, wapatanishi wameonya.

Alitarajiwa kuwasili siku ya Jumatatu kuchukua wadhfa wa makamu wa rais katika serikali mpya ya muungano.

Ni swala muhimu katika makubaliano hayo linalolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka miwili.

Marekani imesema kuwa imesikitishwa na hatua ya Machar kushindwa kuafikia ahadi yake.

Upande wa Machar unasema kuwa kuchelewa kuingia kwa Machar kumesababishwa na mipango na maswala mengine ya usimamizi na kwamba alipanga kurudi siku ya Jumatano.

Taarifa kutoka kwa serikali siku ya Jumanne ilisema kuwa kurudi kwa Machar kulicheleweshwa kwa sababu alitaka kuingia na vifaa vikali vya kijeshi.

Chanzo:
BBC
 
Wangemruhusu tu aingie na silaha na majeshi anayotaka, maana inaonekana hana imani na raisi wa sudan kusini. wangekaa wakubaliane majeshi ya riek machar yaunganishwe na majeshi ya taifa liwe jeshi moja, lakini kwa staili ya mtu kuwa ma majeshi yake hakuna amani hapo
 
Huyu karibu atatumbuliwa west wanahitaji mafuta ya South Sudan yeye bado anataka vita subiri yatamtokea ya Savimbi.
 
Nchi ina mafuta lakini tamaa inawasumbuwa hawa watu.

Waelewane tu wajenge nchi yao au tukawalinde
 
Wasudan kusini walidanganywa wajitenge na Sudan ili wawe huru, kunufaika na rasimali na kuishi kwa amani. Waafrika sijui tumerongwa na nani maana baada ya July 1 wasudani walitarajia mwanzo mpya lakini ikaishia kuwa uwanja wa mapambano Uhasama unasuluhishwa leo ni ushahidi tosha kuwa waafrika tuna laana ya kung'ang'ania madaraka , waliungana wakidai Uhuru sasa wameupata wamegawanya nchi kisa kutaka uongozi.
 
Vipi hapa hakuna mkono au ushawishi wa Marekani?
 
Huyu karibu atatumbuliwa west wanahitaji mafuta ya South Sudan yeye bado anataka vita subiri yatamtokea ya Savimbi.

Na kweli tupu asipotumia mwanya huo wa muafaka atakuja kujuta! Anadhani ndani ya Makamanda wake hakuna anayeuhitaji Umakamu wa Raisi?
Usipocheza vizuri karata ya kisiasa unadondokea Pua
 
Yuko Sahihi. Muasisi wa Taifa lao Mzee John Garang aliuawa kwa Kuhujumiwa angani.

Machar anajua akirudi bila ya Jeshi na Watu Wake Salva kiir anaweza akam sokoine!
 
wazee sudani kusini kuna pesa ni hatari namuomba machal aendelee kuzingua ivo ivo, kule ukipeleka hata maji ya kilimanjaro unarudi na mpunga, ila inabidi usiwe muoga muoga!
 
Hapo ndipo tunashuhudia upuuzi wa viongozi wa kiafrika....sisi huku afrika hatuna viongozi kwa maana ya viongozi...bali tuna watawala waliopo madarakani kwa maslahi yao na sio ya wananchi....
 
Huyu karibu atatumbuliwa west wanahitaji mafuta ya South Sudan yeye bado anataka vita subiri yatamtokea ya Savimbi.
Thubutu! Wachina walishawahi. Wamechukua karibu visima vyote na ndo hao wanaleta kila aina ya silaha ili wenyeji amalizane nao waendelee kuchota mafuta na kuuza zana za kijeshi.
 
nani yuko nyuma ya machar, nani anamfadhili silaha na wanajeshi. tumewakaribisha EAC yy anaendelea kuwatumikia mabwana zake. hajitambui huyo,
 
Thubutu! Wachina walishawahi. Wamechukua karibu visima vyote na ndo hao wanaleta kila aina ya silaha ili wenyeji amalizane nao waendelee kuchota mafuta na kuuza zana za kijeshi.

wanampa nani silaha, wekavizuri hoja ilituelewe vizuri.
 
Hili jizee, sasa makamu wa rais awe na jeshi lake ili iweje, hawa haitakuja siku waishi kwa amani hadi kuzimu.
 
Amani ni kitu kidogo mno na ambacho si gharama kuwa nacho ila consequences za kuipoteza ni kubwa sana...bad enough wanasiasa wanaendelea kutumia mwanya wa kuwa na ushawishi kwa kuendelea kuivuruga Amani!
 
Back
Top Bottom