Suala la utafutaji katiba mpya lisitishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suala la utafutaji katiba mpya lisitishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mangifera, Dec 1, 2011.

 1. m

  mangifera Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kufuatilia kwa kina swala la uundwaji wa katiba mpya ukiwemo mchakato wa kuunda hadi kuisaini sheria mpya ya katiba, nimegundua kuwa hakuna mwenye nia ya kweli (utashi wa kisiasa) katika uundwaji wa katiba mpya. Hii imejionyesha wazi kwa wanasiasa na hata kwa mkuu wa nchi mwenyewe hasa pale alipoongea na wanasiasa wenzake na akaamua kuisaini muswada kama ulivyo, bila mabadiliko. Pia hakuona haja ya kuongea/kuwasikiliza makundi ya kijamii kama jukwaa la katiba na wengineo, ambao mawazo yao hayana mtizamo wa siasa za vyama kama yeye na wanasiasa wenzie!

  Pia kitendo cha wanaCCM(wabunge) wote kuwa na "kauli moja" katika kuupitisha muswada kunaonyesha wazi kuwa walipanga hivyo kwa maslahi ya kundi lao. Maana haiingii akilini watu zaidi ya mia mbili muwe na akili na maamuzi yanayofanana!!

  Kinachotaka kuundwa hapa ni katiba ambayo itawawezesha watu wa kundi fulani (pengine si chama kwa ujumla wake) kufanya mambo yao kwa muda wa miaka kadhaa kwa mgongo wa katiba ambayo wameiunda wenyewe kwa sheria yao wenyewe!!
  KUTOKANA NA MAONO HAYO HAPO JUU, NASHAURI MCHAKATO MZIMA WA UUNDWAJI WA KATIBA MPYA UFUTILIWE MBALI KWA SASA HADI HAPO VIONGOZI WATAKAPOKUWA NA UTASHI WA KWELI WA KUTAFUTA KATIBA YA WATANZANIA NA SI YA MAKUNDI YA WATU.
   
 2. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa ndugu yangu viongozi hao hao ambao hawana utashi wa kuandika hiyo katiba mpya ndiyo hao hao wameamua kuandika katiba hiyo kama wanavyotaka wao. Ukisema zoezi hilo lisitishwe sasa utakuwa unamwambia nani zaidi ya hao hao viongozi waliamua kuandika katiba kwa maslahi yao.

  Cha msingi hapa ni kupiga kampeni ya kuwataka wananchi wa tanzania wapinge hili zoezi kwa njia ya kutokwenda kwenye mikutano ya kukusanya maoni itakayoitishwa na tume ya kuandika hiyo katiba. Na kama wananchi hatakwenda kutoa hayo maoni basi tuone watawala watafanya nini.

  Lakini kama kuna wananchi watajitokeza hata kama ni wachache basi katiba itaandikwa tu kwa msingi kuwa kuna maoni yamekusanywa. Na huku ndiko tunakwenda, kutakuwa tu na watu wataende kutoa maoni hata kama kwa njia ya kulipwa. Si uliona wale vijana walivyojitokeza pale Karimjee Hall siku zile za kujadili muswaada. Kuna walisema walihimizwa kufanya hivyo na viongozi wa chama fulani ingawa wenyewe walikuwa hata hawajui maana ya kwenda pale.

  Pia hiyo kura ya kupitisha hiyo katiba baada ya kuandikwa itahitaji zaidi ya 50% tu ya watu watakaopiga kura kutoka kwenye daftari la wapiga kura bara na zanzibar. Sasa hata kama wapiga kura wakaojitokeza watakuwa watu 1000 na kati hao 501 wakapiga kura ya ndiyo basi hiyo itakuwa ndiyo katiba mpya ya watanzania wote zaidi ya milioni 40.

  Hivyo ndiyo sheria aliosaini rais Kikwete juzi inavyosema.
   
 3. O

  Okinawa Senior Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kikwete kazoe kusaini sheria bila kuisoma.
  Wenzie wa CDM walimwambia ausome kwanza auwelewe ndo ausaini huo mswada.
  Lakimi mimi siamini kama aliusoma.

  Wandugu si mnakumbuku ule mswada wa gharama za uchaguzi alivyochomekewa vitu yeye akausaini tu bila kuusoma !
   
 4. G

  Galinsanga Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
   
 5. G

  Galinsanga Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inayumkinikaje kutegemea hao waliopo wasihusike??? Tafakari , na uchukue hatua sahihi!!!
   
Loading...