Suala la katiba mpya suruhu ni kuanza upya

Suala la katiba mpya suruhu ni kuanza upya

Byendangwero

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Posts
871
Reaction score
56
Kwa maoni yangu mchakato wa kupata katiba mpya ulikwenda tenge pale ambapo sheria iliyotungwa kusimamia mchakato huo ilipoteua wabunge wasasa na wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa wabunge wa katiba moja kwa moja. Uamuzi huo ulikuwa ni wa makosa kwasababu wabunge hao hawakuchanguliwa na wananchi kwaajili ya kazi hiyo, Na zaidi ya hapo uhai wa bunge bunge la katiba uanapashwa kufikia hatma yake baaba ya kupitisha katiba husika, hii ikiwa ni pamoja na mbunge mmoja mmoja anayeunda bunge hilo. Lakini ukweli ulivyo, ni kwamba wabunge hao na wajumbe wa baraza la wawakilishi wanatarajiwa kuendelea na kazi yao ya ubunge baada ya bunge la katiba kufikia hatma yake. Baya zaidi wengi wao wanategemewa kugombea katika muhura ujao. Katika hali hiyo,watu hao hawezi hata kidogo wakachangia kwenye mjadala wa katiba mpya kwa uhuru kabisa bila ya kuzingatia maslahi yao binafsi. Ni kwasababu hiyo ingelikuwa vema, bunge la katiba la sasa likavunjwa, na sheria ya mchakato wa katiba mpya ikafanyiwa marekebisho kuruhusu wabunge wa bunge hilo wachaguliwe moja kwa moja na wananchi. Baada ya hapo mchakato huo uendelee kwa msingi wa msimamo wa UKAWA
 
Back
Top Bottom