Suala la elimu sasa lipewe kipaumbele na Serikali

Suala la elimu sasa lipewe kipaumbele na Serikali

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Serikali imefanya makubwa kuhusu maendeleo mfano, Vituo vya afya, Barabara, Hospitali, SGR, Umeme etc. Sasa ni wakati wa Serikali kuhamia kwenye ELIMU. Sekta ya elimu inakabiliwa na upungufu mkubwa kuanzia na Walimu, Madarasa, vyoo, nyumba za walimu n.k.

Ni vyema Serikali ikatumia mtindo wa FORCE ACCOUNT kukamilisha mapungufu niliyoyaelezea hapo juu. Kwa nchi nzima tuna takriban shule za msingi zipatazo 15,000 hivyo kama Serikali ikatoa fedha za kujenga kila shule kujenga madarasa 20, nyumba za walimu 20, vyoo vya matundu 20 kwa kila shule kama ilivyotumika kwenye ujenzi wa Vituo vya Afya.

Natumaini hakutakuwa na upungufu kwa muda wa miaka 10 ijayo. Kila mwaka watoto wanaoanza shule wanaongezeka hivyo inatakiwa Serikali kuchukua hatua stahiki.

Jambo la pili ni kuhusu upungufu wa walimu katika shule zetu za Sekondari. Watoto wengi wanaofaulu kwenda sekondari hawapati elimu inayofaa kwa sababu ya ukosefu wa walimu hasa wa sayansi.

Tunaimba kauli mbiu ya viwanda lakini hatuna walimu wa sayansi. Kuna shule nyingi za vijijini hawana walimu wa Hisabati, kemia, fizikia, bayolojia nk. Ni vyema serikali ikaliona hili.

Wengi wa walimu wa sayansi wenye shahada wako mitaani na hawana ajira. sasa ni wakati muafaka juhudi zote zikahamia kwenye sekta ya elimu.
 
Back
Top Bottom