tourmaline21
New Member
- Jul 30, 2015
- 1
- 0
Tangu Rais wetu JPM aingie madarakani kumekuwa na jitiada mbalimbali toka kwake za kuirudisha nchi kwenye mstari, jambo ambalo kwa ujumla wake ni la kuungwa mkono kwa kila mzalendo wa nchi bila kujali maswala ya kiitikadi. Hatahivyo serekali ya awamu ya tano inapofanya jitihada kuweka mambo mbalimbali sawa, namwomba Rais JPM hili suala la bomoabomoa ya makazi hasa ya watu wanyonge litazamwe kwa macho matatu ( sheria, haki, busara ) Kwamba kwa kiasi gani kweli mhusika alivunja sheria. Kuna wakati mamlaka fulani kwa uzembe wanashindwa kuzingatia kikamilifu sheria Na.4 na Na.5 ya mwaka 1999 ambayo pamoja na mambo mengine , inataka serekali/mamlaka husika kuwashirikisha/kuwahusisha kikamilifu wananchi wa sehemu husika kabla ya kutwaliwa ardhi yao kwa maslai ya umma. Inapotokea wananchi tena wanyoke wamefanya maendelezo kwenye ardhi yao iliyotwaliwa kimyakimya bila ushirikishwaji wala bila fidia kadiri sheria tajwa hapo juu inavyotaka, kuwaita wavamizi na kuwavunjia makazi yao ni kuwaonea na kwenda kinyume cha sheria. Katika mazingira mengine ya mjini, mfanyabiashara mdogo mama lishe/baba lishe/mmachinga au mstaafu baada maangaiko ya miaka mingi ya kupata makazi, anapoaminishwa na mamlaka halali za serekali kimaandishi kwamba eneo ni halali na kupewa kibali cha ujinzi na mamlaka halali ya serekali, kumbomolea kwa kumwita mvamizi aliyekiuka sheria za nchi nafikiri si haki. Kuwaacha watendaji/serekali/mamlaka husika kutokuwajibika kwa hili si haki hata kidogo. Kwa wale bomoabo
moa inapowakuta katika mazingira tajwa hapo juu na hasa kwa wanyonge ambao ni wazi hawana nguvu yoyote ya kupindisha sheria, ndipo ninapomwomba Rais wetu JPM na serekali yetu ya awamu ya tano kulitiza suala la bomoabomoa kwa macho matatu-sheria, haki na busara ili tukawe na mwanzo nzuri wenye kheri na baraka kwa serekali yetu awamu ya tano. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU UENDELEE KUMJALIA MOYO WA UJASIRI, HEKIMA NA BUSARA katika kuliongoza TAIFA letu Rais wetu JPM.