Suala la Bima za pikipiki

Suala la Bima za pikipiki

ndemeyejr

Member
Joined
Oct 31, 2016
Posts
18
Reaction score
19
Habari,kuna kero naona hapa Runzewe- Bukombe,Geita,baada ya waziri wa mambo ya ndani Mh.Kangi Lugola kutolewa kwenye Wizara hiyo na kukaliwa na Mh.George Simbachane,watu wa bima ,mfano Bumaco company wameanza tena kamatakamata ya pikipiki.

Je,waziri wa sasa ameruhusu tena pikipiki kukamatwa kama haina Bima? Waziri aliyepita alisema ,Pikipiki ya kukamatwa ilipaswa kuwa 1.Uliyosabibasha ajali 2.Iliyoibwa 3.Iliyohusika katika uharifu.

Je, sasa mambo mbona yamebadilika bila kusikia kauli ya waziri mwenye dhamana.Naomba kuwakilisha dukuduku yangu kwa Waziri.
 
Mjomba hakuna waziri anaeweza kuruhusu utumie pikipiki bila bima,ni kwa usalama wako. sema hivi ukamataji wao labda si mzuri na ni bora nyie huko.

Sisi huku dar mjini kuingia mpaka uwe na kibari, miezi 6 ni elfu 90000 nahisi mwaka ni laki na 60, haijalishi ni bodaboda au unatumia kwenda kazini,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom