sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,734
- 1,150
Kwanini tunaimba mshikamano na umoja,kwanini tuna tekeleza Operation ya NO REFORMS,NO ELECTION, kwa sababu tumechoshwa na ghiliba ya mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi kwa zaidi ya miongo mitatu.
CCM haina nia ya dhati kuruhusu/Kutengeneza mianya ya haki itakayo kiweka chama hicho nje ya mamlaka na madaraka iliyo nayo.
Tumeshiriki chaguzi nyingi kwa zaidi ya miongo mitatu,tukiwa tumesimama kwenye Yes election,no reforms tukageuzwa mbuzi wa kafara kwenye karamu ya mitambiko ya madaraka,matokeo yake mamlaka madaraka ya wananchi kuiweka serikali madarakani imeporwa na kuangamiza ustawi wa Taifa hili.
Madai ya mabadiliko(reforms) ya sheria na kanuni za uchaguzi,yanachagizwa na udhaifu wa katiba ya watu wasiozidi ishirini iliyobeba maono ya Watanzania zaidi ya milioni sitini,yanayokinzana na wakati uliopo,iliyoitwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Katiba hii imeendelea kutoa mwanya kwa CCM kujiamini ina haki na nchi hii kuliko chama chochote,na kutoa fursa ya kuuchezea uchaguzi watakavyo.
Ndiyo maana Maridhiano yeyote na CCM watakayo yaafiki ni yale yatakayo ihakikishia kubaki salama madarakani hata kwa uhai wa damu za Watanzania.
Tumeona dhamira ya dhati ya CCM kutoyakubali maridhiano yanayochochea uhalali wa kidemokrasia utakaowapa likizo,pamoja na mazungumzo kuvunjika,Bado mapendekezo ya CHADEMA hayakufanyiwa kazi hata machache miongoni mwa yale ya kiuchaguzi kuonyesha dhamira ya dhati iliyobeba msingi mkuu wa hoja katika maridhiano hayo na ustawi wa Taifa.
Dhamira yao ovu,imebebwa na kejeli ya Mwenyekiti wao kuwa Tanzania inahitaji elimu ya katiba kwa miaka mitatu,ndipo mabadiliko ya katiba yafanyike ilihali mchakato wa rasimu ya katiba ilifikia hatua ya kura za maoni.
Kwa mantiki hiyo utaona kuwa Mbinu yeyote hata kama haina mikono yao,lakini inatoa mwanya wa wao kuendelea kubaki madarakani kwao ni ushindi mkubwa sana katika maziko ya demokrasia.
Na kwa kuwa ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa mamlaka ya wananchi kuiweka serikali madarakani. Kilichobaki CCM kuichezea hiyo haki kwa mbinu chafu ili iendelee kubaki madarakani.
Ukizingatia katiba imefungwa mdomo kuhusu hatua gani itachukuliwa kudhibiti wahalifu wanaopora haki iliyotolewa na ibara hiyo ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wananchi wamenyimwa hata Haki yao hiyo ya kutumia uchaguzi, kuiweka serikali waitakayo madarakani kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
kwa msingi huo CCM itaendelea kuchezea uchaguzi na ghiliba nyingi,kulinda hadhi yao haramu na kutumia mwanya huo wa kikatiba unaotoa haki na kunyang'anya kwa wakati mmoja.
Wapinzani wataendelea kuwa sehemu ya CCM kujinadi duniani,kuwa nchi ya kidemokrasia chini ya mfumo wa vyama vingi kwa kukubali kushiriki chaguzi zinazokiuka misingi ya kidemokrasia kwa mfumo wa uchaguzi wa chama kimoja na katiba isiyoakisi mfumo wa vyama vingi.
Tukisema tunataka mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi lugha iwe moja,miruzi mingi humpoteza mbwa, haiwezekani kuingia kwenye ushindani tukiwa na lugha zinazokinzana.
Turejee chaguzi zetu,kuna haki! Kama hakuna,haki inaombwa au inatafutwa?
Hakuna movement za kuomba haki duniani,Mahatima Ghandi anajua,Martin Ruther anajua na Mandela halikadhalika,zipo movement za kudai haki tu,sisi Chadema tutaidai kwa kuzuia chaguzi zinazowaweka CCM madarakani kwa mbinu chafu na kuzuia haki isitendeke.
Chaguzi zetu zimekuwa vita,watu watwezwa utu wao,maisha yanapotea badala ya ustawi wa wananchi,na ikitokea kigezo cha umwagaji damu ndiyo chachu ya ushindi kwenye uchaguzi,lazima tuchukue tahadhari kwa kuzuia uchaguzi dhidi ya vwahuni wa madaraka.
Serikali imeendelea kutumia mbinu chafu kuwashughulikia wapinzani wake wanapinga mifumo kandamizi,kwa kuwakamata mara kwa mara viongozi wa CHADEMA na kuwabambikia zinazopeleke hukumu ya kifo ili kuuwa ndoto za vuguvuguvu la mabadiliko.
Wahanga wa mfumo huo kandamizi ni panoja na Mbowe aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kwa kutuhumiwa kuwa Gaidi na kusota jela kwa zaidi ya miezi sita,sambamba Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Lissu kutuhumiwa Mhaini anayedai mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi.
Kama kuongea, tumeongea ndani ya uchaguzi kudai haki za wapiga kura kuheshimiwa maamuzi yao kwenye uchaguzi kwa zaidi ya miongo mitatu,kuturudisha kwenye maongezi ya kudai haki tukiwa ndani ya uchaguzi ni bora maradufu kuzuia uchaguzi huo na kudai haki nje ya uchaguzi. Tukifanya hivyo hakika tutakuwa tumeweza kuongea lugha moja wakatuelewa.
Movement zote hazikuwahi kutokea duniani ila zilipojitokeza kwa mara ya kwanza zilileta tija. Kwa hiyo kuzuia uchaguzi haijalishi kama ilishawahi kufanyika duniani au la!,kwa kuwa lengo kuu ni kulinda haki za wadau wa uchaguzi na wenye mamlaka ya kuiweka serikali madarakani ambao ni wananchi na kulinda uhalali wa haki za binadamu kulindwa kwa mujibu wa mkataba wa amani wa Vienna, Tanzania ikiwa mwanachama wake.
Turudi kwenye chaguzi zinazopigiwa chapuo kuwa mapambano ya haki/reforms yapatikane ndani ya uchaguzi, huku tukifanya tathimini ya wahanga wa uchaguzi waliopoteza maisha yao toka kuasisiwa mfumo wa vyama vingi 1992 .
Zaidi ya mamia ya wapinzani wameangamizwa na kuacha familia zao zikitaabika,lakini chaguzi zikionekana za kidemokrasia,kinyume kabisa na maudhui ya chaguzi huru,wazi na haki.
Hatuwezi kuwa na uchaguzi huru,ambao Mwenyekiti wa CCM ndiye anayesaini sheria kandamizi,na mteule wake waziri wa Tamisemi anatunga kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa.
Tume ya Taifa ya uchaguzi imepoteza uhalali ndani ya chaguzi zenye mfumo wa ushindani wa kisiasa wa vyama vingi,imeendelea kuwa dalali wa batili dhidi ya maamuzi halali ya wananchi ambao ndiyo wenye kutoa mamlaka na madaraka ya serikali kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 8 ya mwaka 1977
Ikiwa marekebisho ya kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa yalifanyika mwaka 2024,kanuni hizo zikatumika kuendesha uchaguzi huo,na ukiukwaji mkubwa wa kikanuni ukafanyika kwa kiwango kikubwa sana ikiwa pamoja na kanuni kuwalinda wasimamizi wasaidizi kutokuchukuliwa hatua za kisheria kutokana na kusimamia uchaguzi huo,kwa hali hiyo unawezaje kutaka kwanza uchaguzi ndiyo upambanie reforms.
Mtaa mmoja tu wa Mkongoni,kata ya Mkuza Jimbo la Kibaha Mjini imetumika nguvu kubwa ya kulazimisha masanduku kuingizwa baada ya kukamatwa na mawakala, viongozi wetu wakawekwa ndani,mbele ya usalama wa Taifa na jeshi la Polisi,na bado masanduku yenye kura fake yakaingizwa na kuhesabiwa yakiwa yamepigiwa kura kwa wagombea wa CCM tukiwa ndani ya uchaguzi,tunawezaje kutaka uchaguzi usio na reforms, kwa kushinikiza tutafute reforms ndani ya chaguzi.
Unawezaje kuingia kwenye uchaguzi unaosimamiwa na wenye kinga ya kuvuruga uchaguzi ambao ndiyo wasimamizi wa uchaguzi kwa maana ya Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa na Rais wakiwa chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI ambao pia wanajibika kwa waziri aliyetunga kanuni hizo za uchaguzi.
Kwa msingi huo, maazimio ya mkutano mkuu wa CHADEMA yaliyopitishwa na wajumbe,yaliazimia bila mabadiliko hakuna uchaguzi "NO REFORMS, NO ELECTION"
Msingi wa waraka wa G55 unabebwa na neno ushauri kwa chama,kutoa ushauri kwenye mifumo ya Kidemokrasia ndiyo kuishi Demokrasia yenyewe. Kutoa maoni haijengi dhana ya Usaliti,usaliti ni dhamira au utashi unaolenga kushinikiza ulazima wa jambo lako,kinyume na utaratibu wa uwasilishaji hoja kwenye vikao.
Tukitazama maudhui ya ushauri wa G55 huenda una hoja nzuri za msingi sana,lakini uwasilishaji wake uliojaa shinikizo na kutengeneza timu ya ushauri inayolazimisha ushauri huo kujadiliwa ndiyo unaotia shaka,nini hasa dhamira yake, ukizingatia circumstances zote chama kilichopitia kwenye Chaguzi hizi.
Mgongano wa mawazo kwa taasisi yeyote ndiyo afya ya mjadala wenyewe, halikadhalika ushauri pia.
Kwa kuwa ushauri haupaswi kuwekewa shinikizo kama ilivyo sasa kwa kulazimisha kupitia press conference tatu,kukiponda chama na program zake kwa kuwa tu,kuna dhamira binafsi nje na matakwa ya chama hapo ndipo panapotia shaka, ukizingatia watoa ushauri kwa asilimia kubwa ndiyo wajumbe wa mkutano mkuu ambao kupitia kwayo walipitisha maazimio hayo kwa kura ya sauti kwa ajili ya utekelezaji kwenye mkutano mkuu uliofanyika tarehe 21/01/2025.
Kwa mantiki hii kuna swali la kujiuliza,kwanini "No reforms no election" ushauri au shinikizo linakuja leo nje ya vikao,baada ya operation kuchukua kasi!
Kama mtakumbuka,mkutano mkuu wa CHADEMA ulifanyika 21/01/2025 moja ya agenda muhimu sana ilikuwa ni taarifa ya Baraza kuu,agenda namba 4.
Agenda hii ilizungumzia takwimu mbalimbali za kiuchaguzi toka mwaka 2019 /2024. Lakini pia ilizungumzia hali ya kisiasa nchini kwa kipindi cha miaka mitano,2020/2025.
Ukisoma taarifa ya baraza kuu 3.10.3 MAENEO YA MAREKEBISHO YA KATIBA(MINIMUM REFORMS) ilisisitiza kuwa kuna maeneo kadhaa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuboresha mfumo wa uchaguzi kama ifuatavyo;
(a). Hoja ya uwepo wa mgombea huru Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hoja ilisisitiza kufanyiwa marekebisho ibara ya 39(2) ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977. Ambayo inasema;
"Bila kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoni yake,kuamini dini atakayo,kushirikiana na wengine na kushiriki shughuli za umma kwa mujibu wa sheria za nchi,mtu yeyote hatakuwa na sifa za kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kama si mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa".
(b). Mgombea wa urais kutangazwa mshindi baada ya kupata kura nyingi(simple majority) kushinda Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baraza kuu lilishauri kufanyiwa marekebisho ibara 41(6) ya Katiba ya JMT ili kuondoa sharti la Mgombea wa kiti cha Urais kutangazwa mshindi baada ya kupata kura nyingi (simple majority) na kuweka utaratibu mwingine.
(c). Matokeo ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhojiwa mahakamani. Hoja hii imesisitizwa na kikao cha baraza kuu kufanyiwa marekebisho ibara ya 41(7) ya Jamhuri ya Muungano ili kuweka utaratibu wa namna ya kuhoji matokeo ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ambapo Kwa Sasa ibara hiyo inakataza matokeo ya Urais kuhojiwa Mahakamani.
Pamoja na kutaka kufanyika marekebisho baraza kuu liliainisha mapendekezo manne kwa ajili kupata uhalali wa kushinda Urais huo;
(i). Kupata haki ya kuhoji matokeo ya Urais mahakamani kupitia wagombea/mgombea/wapiga kura,
(ii). Maombi ya kuhoji matokeo hayo wafike a neo yaletwe ndani ya siku 7 tangu kutangazwa kwa matokeo ya Urais,
(iii). Shauri hilo lisikilizwe na Majaji wa Mahakama ya Rufani wasiopungua saba wakiongozwa na Jaji mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuamuliwa ndani ya siku 14 tangu shauri kuletwa.
(iv). Ikiwa mahakama ya Rufani itajiridhisha na kutoa uamuzi kufuta matokeo ya uchaguzi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,uchaguzi mpya utaitishwa ndani ya siku 60 tangu tarehe ya kutolewa hukumu ya Mahakama.
(d). Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua madaraka. Kwa mujibu wa ibara ya 42 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inamtaka Rais kushika madaraka mapema iwezekanavyo,ikimbidi kabla ya siku 7.
Kimsingi jumla ya hoja 25 zilizopendekezwa na baraza kuu zinatokana na uchaguzi wa Urais,Ubunge na udiwani,ambayo yalipaswa kusimamiwa kwa kiwango kikubwa ili reforms hizo zifanyike katika maintenance of democracy.
Pia,baraza kuu liliorodhesha mambo mengi ikiwemo uchaguzi wa serikali za Mitaa na uchafuzi wake katika kuuwa misingi ya demokrasia na utawala bora.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na sheria mbalimbali zinazohusu masuala ya uchaguzi na usimamizi wake.
Hivyo baraza kuu lilisisitiza kuwa kwa kuwa tume ya Taifa ya uchaguzi ni zao la Katiba ibara ya 74 ya katiba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kutaka kutunga sheria ya kuboresha mazingira ya usimamazi wa uchaguzi nchini lazima kwanza yafanyike mabadiliko madogo ya katiba ili kuyaingiza maboresho hayo ndipo uweze kutunga sheria husika.
Pamoja na mapendekezo hayo,sheria za uchaguzi zilizotungwa mwaka 2024,mapendekezo yote ya chama yenye tija yalitupwa mbali kuonyesha dhamira ovu ya serikali na chama kilichoko madarakani ambacho Mwenyekiti wake ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa mnufaika wa sheria hizo kwenye uchaguzi huu.
mapendekezo hayo ni kama ifuatavyo;
i. Serikali iwasilishe muswada Bungeni wa kukwamua mchakato wa katiba Mpya pamoja na Mwelekeo (road map) wa kila hatua mpaka ipatikane Katiba
Mpya kwa kuzingatia mwafaka wa
Kitaifa.
ii. Serikali iwasilishe Bungeni muswada wa kufanya marekebisho ya mpito ( minimum reforms) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ili kuwezesha kufanyika
uchaguzi huru na haki baada ya
kuondoa mapungufu ya kikatiba
yaliyopo Sasa yanayoathiri sheria
zinazoenda kutungwa.
iii. Serikali iwasilishe Bungeni muswada ambao,pamoja na mambo mengine ya uchaguzi huo,Tume ya Taifa ya uchaguzi ipewe mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa na sio kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kwa kanuni ambazo zinatungwa na Waziri wa Nchi anayehusika na TAMISEMI.
iv. Muswada wa marekebisho ya sheria za Vyama vya siasa (Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyorekebishwa mwaka 2019 na sheria Gharama za uchaguzi) uondolewe kwa sababu hautatui changamoto zilizopo sasa na badala yake muswada wa sasa unampa mamlaka zaidi Msajili wa Vyana vya Siasa ambapo vyama vitabanwa zaidi na Ofisi ya Msajili ambayo haipo huru kwa mujibu wa katiba,ilihali muswada huo umepuuza amri halali ya Mahakama ya Afrika Mashariki,ambapo baadhi ya vifungu viliamriwa kwamba vinakiuka Mkataba wa Afrika Mashariki.
v. Miswada iliyowasilishwa Bungeni tarehe 10/11/2023 iondolewe na kuandikwa upya kwa mujibu wa marekebisho ya mpito ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 yatakayofanyika kama ilivyopendekezwa hapo awali katika aya ya pili ya muundo wa Tume ya uchaguzi.
Pamoja na taarifa mbalimbali ya hali ya kisiasa nchini kwa miaka mitano 2020/2024, kwa kuzingatia kila eneo la kiutendaji maazimio ya kamati kuu yalikuwa kumi na moja.
Azimio la kumi na moja,kamati kuu imeazimia kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 lazima pawepo na marekebisho ya msingi ya Kikatiba na kisheria ambayo yatawezesha kufanyika kwa uchaguzi huru,haki na wa kuaminika nchini. Iwapo marekebisho hayo hayatafanyika,chama kitawaongoza Watanzania kuchukua hatua za kuhakikisha uchaguzi haufanyiki
( "No reforms,No election")
Hayo yote yaliidhinishwa na Mkutano Mkuu wa chama wa tarehe 21/01/2025,kwa Mwenyekiti aliyemaliza muda Wake Freeman Aikaeli Mbowe,kwa kuwahoji wajumbe wa mkutano mkuu kama wameridhia na kama kuna hoja yeyote. Wajumbe wote walitikia ndiyooooo.
Swali, ni sahihi leo hii kuhoji kuhusu utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa na mkutano mkuu wa chama ,ambacho ndicho chombo chenye maamuzi ya mwisho kuhojiwa nje ya vikao rasmi,ilihali nafasi hiyo ya kuhoji ilitolewa kwenye mkutano ulioidhinisha maamuzi hayo!!
Binafsi,naamini kuteleza si kuanguka,turudi kwenye katiba yetu inatuongoza vizuri,tuisome kwa umakini kabla ya kuteleza zaidi na kuzua taharuki.
Pili, wajumbe wanaohoji nje ya vikao walivyoshiriki kuidhinisha Maazimio hayo wanapata wapi uhalali wa kuhoji nje ya vikao,ilihali wao ni sehemu ya walioazimia!
Tatu,wajipime waone kama kuna haja ya kuendelea kushinikiza kujibiwa hoja zao wakati walishapewa nafasi ya kuhoji ndani ya vikao.
Nne,ushauri una mambo mawili,kukataliwa au kukubaliwa,ukilazimisha ujibiwe wakati sababu ya utekelezaji wa maazimio hayo yalishabainishwa wazi,kunazua taharuki inayojenga taswira yenye jambo la siri,nyuma ya pazia.
Mwisho,upinzani una tofauti kubwa sana na ukinzani wa hoja,ukinzani wa hoja ulishapewa haki yake kwa kuhojiwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake,haukutoa matokeo chanya,kinachofanyika sasa ni upinzani ndani ya utekelezaji maazimio ya mkutano mkuu.
Niwaombe viongozi wenzangu turudi kwenye hotuba ya katibu mkuu kuhusu taarifa ya utekelezaji majukumu ya chama kwa miaka mitano,na maazimio yake, aliyoyatoa kwenye mkutano mkuu huenda kuna sehemu tuliteleza,tukajisahau kuhoji.
Mungu ibariki Chadema,Mungu Ibaraiki Tanganyika,Mungu Ibariki Tanzania.
Imetolewa na
Ally Mussa Mjema
KATIBU WA CHADEMA,JIMBO LA KIBAHA MJINI
0746137077