daah umenikimbusha chief yangu ni hii
kuna kipindi nilikua nimeenda kulipa benki kudiposit hela ya mzee kwenye akaunti ya ukoo wao dodoma uko .
basi bwana kufika pale benki nakuta watu wa kutosha na benki bado haijafunguliwa. kuuliza naambiwa ni wanafunzi wa chuo ndo mwaka umeanza wakusoma ila wameongezewa hela ya kulipa ghafla kama 85k
tukaendelea kusubili watu wengi si kitoto.
mda ukafika watu tukazama ndani foleni hadi nje .
alafu wapokeaji wanafanya kazi taratib vibaya .
nilkua kama mtu wa 50 hivi
story yenyewe
mpaka saa6 watu bado utazani asubuhi
mchezo ukaanza watu wa nyuma wanawapa wa mbele pesa wawalipie
kwaio folen ikawa haisogei.
jamaa mmoja akamwabia mhudumu mchezo unaofanyika .
jamaa: asee watu wanalipiana afu wamefika saivi tu tafadhali usipokee zaidi ya slip moja
mhudumu:siwezi kataa kumuhudumia mteja
mhudumu akawa amechochea moto wa mchezo
hapo nshafika kama mtu wa 15 na sweta langu la kijivu.
ghafla nashangaa watu kama 12 wananikabizi pesa na karatasi niwalipie chap chap nikazkamata fresh
nkaendelea kusubili zamu ifike nafika kama mtu wa 8 akili ikanambia (usipotumia akili utakufa masikini mbwa wewe) duh nkashtuka hapa nfanyeje akili ikaja naam
nikatoa laini na memory chap kwenye simu alafu nkamuita mmoja wa walionipa hela nikamwambia anishikie ili niwe huru
baada ya kumpa kweli bhana wakapunguza kuniangalia na kua bize kiasi flan .hapo sasa
mwanaume chap nkavua sweta nikamkabidhi wa nyuma yangu niikabaki na manga nyeupe
mdogomdogo naanza kuelekea mlangoni .ghafla naona mwnga wa jua kwamba tayari niko nje
asee sikumbuki ilikuaje ila nakumbuka tu niljikuta nipo geto na laptop mpya na simu mpya smart.
na mpaka leo sijawahi kusogea kwenye ile benki
NBukipata fursa tumia mbwa ww