Story ya kweli: Jinsi nilivyomtapeli Ngosha

Story ya kweli: Jinsi nilivyomtapeli Ngosha

Jile79

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2009
Posts
17,668
Reaction score
13,271
Leo asubuhi nimepanda daladala kutokea maeneo ya Nyakato sokoni kuelekea Bwiru lakini nikiwa nimelenga kushukia Kirumba sokoni.

Basi kama unavojua nauli yake kawaida ni sh 500 na mimi huwa sipendi kabisa kuwasumbua Kondaz kwa hiyo huwa nina kawaida ya kubeba nauli kamili mkononi.

Nilikua nimeshika mkononi mwangu sh 500 (200 moja na 100 tatu), kwa bahati mbaya ah 100 moja ikadondoka chini.

Nilipojaribu kuchungulia nikaiona kwa chini lkn nisiweze kuichukua kwa sababu ya kubanana sana na abiria wengine. Nilikua nimekaa siti ya nyuma mwisho.

Konda alipotaka nauli yake nikampa ile sh 400 niliyokua nimeshika mkononi na kumwambia nitampa sh100 iliyobaki kwani imedondoka chini na cwezi kuiokota kirahisi.....Konda akanielewa.

Daladala ilipofika mjini Makoroboi km kawaida ikashusha abiria kibao maana watu wanaingia sn mjini kufanya manunuzi na hata kutembelea sehemu mbalimbali pale katikati ya mji.

Nikajikuta nimebaki peke yangu siti ya nyuma ndipo nikaiokota ile sh mia huku konda yuko nje akihamasisha wasafiri wapande kwenye daladala yake.

Mpaka muda huo tulikua tumebaki jumla watu 4 tu ndani ya basi kwa ajili ya kuendelea na safari baada ya wengine kushuka.

Baada ya km dk 3 hivi abiria walikua wameshajaa na konda bila ajizi akamwamlisha dereva wake aondoe gari...Tukaanza safari kuelekea Bwiru.

Nikiwa nimeketi siti ya nyuma pembeni kushoto, kulia kwangu alikuwepo jamaa mmoja ambaye alionekana mshamba lkn mwenye possibility ya kua na pesa pengine baada ya kuuza ng'ombe.....😁😁

Tukasalimiana km ilivo desturi ya sisi Waafrica hususani Watz tukutanapo. Tukabadirishana maneno kidogo ndipo nikagundua yy ni Ngosha na alikua anaelekea Sengerema hukoo....

Baada tu ya daladala kuanza safari km kawaida ya makonda wote walivyo na njaa ya pesa, basi akaanza kuwadai ndugu zake wote nauli (Kaka hapo mbele, anti nyuma hapo nauli, mamkubwa nauli yangu tafadhari, nk).....

Alipofika kwangu nikatoa ile sh 100 niliyomwahidi kumpatia wala hakuniuliza chochote maana alikua anakumbuka (makonda wanakumbukumbu sn usijaribu kujifanya umelipa nauli utaumbuka) nilichomwambia baada ya kudondosha ile coin, huku pembeni kulia kwangu Ngosha akaniangalia na kushangaa kiasi nami nilipomstukia ikabidi nimuangalie na kumuuliza....Mbona km unanishangaa?

Akanambia mbona ni km umempa konda sh 100 tu kulikoni? "Akili za kumfanyia utani Ngosha zikanijia haraka......
Nikamjibu hiyo kwangu ni kawaida kwani silipagi nauli kamili popote nnapokwenda...

Akashanga na kucheka kidogo na kusema labda wewe ni afande au konda ni ndugu yako maana nijuavyo sio rahisi kumlipa konda nauli ndogo kiasi hicho kwa jinsi ninavyowafahamu makonda.....

Nikafikiri haraka haraka alafu nikamjibu kua mimi nina dawa aliyonipa babu na sasa ni miaka 15 imepita nasafiri kwenda kokote iwe kwa ndege, Meri,Basi treni nk napanda kwa nauli pungufu kwa 20% ya nauli halisi...Ikabidi nimweleweshe zaidi kwa calukulesheni kua kwa mfano km nauli ni sh 500 mimi natoa sh 100 na inapokelewa bila shaka yoyote na kk kwa mfano nauli ya Mwanza- Dar ni sh 50,000 basi mimi hutoa 10,000 tu na wanachukua......

Akaniuliza iwapo inawezekana nimsaidie na yy hiyo dawa iwe inamsaidia wkt wa kusafiri.....

Nikamwambia kwa kua umekua rafiki yangu nitakusaidia japo sifanyagi hivyo kwa mtu ambaye sijamfahamu vizuri ila pia nikamtahafharisha atunze sana siri nitakayompa... Nikamwambia nikikupa dawa hata hapo kivuko gharama yake ni sh1,000 Ila ww utapia 200 na wataipokea bila shida na utaendelea hivyo hivyo kwa usafiri wowote maisha yako yote...

Unanisaidiaje sasa Kaka yangu?.. akaniuliza kwa hamasa fulani hivi.

Nikamjibu hii kwa ww nitakufanyia sh 700,0000 tu. Akajitetea na kuniomba nimpunguzie tukakubaliana anilipe sh 500,000 ili nimfanyie dawa husika. Akavutika na hiyo deal fasta akavuta mpunga kutoka kwa begi lake kuukuu anachomoa bunda ya 1,000,0000 akahesabu zangu 500,000 akanikabidhi nami nikazipokea bila kuhesabu fasta nikazitia kwa mfuko wangu.

Nikafiria cha kufanya hasa kuhusu namna ya kupata dawa, ghafla nikakumbuka kua nina kipande cha sigara mfukoni mwangu. Basi nikakichukua na kukiweka kwenye leso yangu nikafikicha na kutengeneza unga ambao nikampaka kwenye paji la uso na nyengine nikampa na kumwambia afunge kwenye kitambaa achanganye na pesa zake mambo yatakua poa maisha yake yote.

Tukaagana maana alikua anashukia sokoni huku mm nikiendelea na safari ambapo nikaenda kushukia maeneo ya mbelenya kona ya bwiru.

Baada ya kushuka nikaingia bar fulani nikatafuta demu mkali tukaanza kutumia...

Sijawahi kutapeli maishani mwangu Ila Nahisi kunogewa na kilichotokea.... Hapa nafikiri ni namna gani naweza kumtapeli raia mwingine kimasihara namna hiii? Kwani hii inetokea just by coincedence...

KARIBUNI WADAU
 
Halafu ndefu mno,kakosea mno herufi,atakuwa ameiandaa kwa muda usiochini ya mwezi mmoja kabisa aisee..!
Hahaaaa.......acha unaa...hiyo imeandaliwa fasta baaada tu ya tukio✍️✍️
 
Back
Top Bottom