Stori ya maisha yangu

Emmanuel180

JF-Expert Member
Dec 17, 2019
342
626
"Nakumbuka nilipata kuitwa kwenye interview ya kazi ya mradi wa mwendokasi, basi kuna rafiki yangu alikuwa Tanga akahamia Dar es salaam kikazi, ni mchungaji. Nikawasiliana nae akasema nitafikia kwake kwa kipindi cha mwanzo nikianza kazi nitapanga chumba.

Basi kwakuwa hali ya uchumi haikuwa sawa na natakiwa nije Dar haraka iwezekanavyo, nikauza simu yangu ilikuwa Huawei Ascend Y500 nikapata pesa ya nauli na kununua kasimu kadogo kwa ajili ya mawasiliano.

Nikaanza Safari ya Dar, ilikuwa Jumamosi nakumbuka.

Nimefika maeneo ya Mbezi nikamcheck jamaa yangu akawa hapatikani na tulikuwa tunawasiliana njia nzima, nikajua labda ni mtandao tu. Basi nikafika Ubungo saa 3 usiku na jamaa bado hapatikani.

Nikalazimika kulala pale stand. Asubuhi namcheck bado hapatikani, ikabidi niende kanisani kwao nikijua nitaonana nae ila wapi.

Kwakuwa sikuwa mwenyeji sana ikabidi nibaki kanisani pale mpaka usiku. Usiku ulivyofika nikaona sio kesi, nikalala pale pale na wachungaji waliokuwa wanasomea.

Kanisani kwa Gwajima wakati ule palikuwa na wachungaji wengi wanasomea nikajiunga nao kwenye usiku wa maombi kisha tukalala zetu kule juu.

Asubuhi kukakucha, Jumatatu nikaenda kwenye interview bahati nzuri nikapita, ila pia bahati mbaya nikakwamishwa na boss fulani so mchongo ukawa umegoma.

Sikuwa na namna, nikakata tamaa ikabidi nimcheck mzee wangu anitumie nauli nirudi home tu. Kupiga simu mzee akasema hapo ndio mjini, kaza.

Akaniambia kuna mzee wako mmoja nikuunganishe nae ufikie kwake. Basi nikapewa mawasiliano yake akanielekeza nikaenda mpaka pale, kwakuwa sikuwa na nauli ikabidi tu nitembee kutoka Ubungo mpaka Ilala msimbazi centre,
nilifika kwa maelekezo ya wadau njiani. Nashukuru nilifika na akanipokea vizuri tu.

Nikaanza kuishi pale. Changamoto zilikua nyingi na nzito ila sikuacha kuamka na tumaini kila asubuhi. Basi nikawa naangalia na kutafuta marafiki mtaani pale nakaa kaa nao.

Kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Vincent, alikuwa anafanya kazi posta ikawa asubuhi naenda nae mimi nakaa nje mahali mpaka mchana narudi nae home ananinunulia chakula na nauli ananipa.

Nilikuwa najisikia vibaya sana kuamka na kukaa kaa tu pale nyumbani.
Ilikuwa bora nitoke nionekane nimeenda kutafuta.

Sasa ikawa nikiwa kwenye gari naangalia yale mabango ya wanaojihusisha na mambo ya ICT, nachukua namba nikifika home napiga naelezea taaluma yangu na kuona kama kuna mchongo.

Basi nikawa nafanya hivyo mara kwa mara, wengine nikawa naomba hata nifanye kazi free. Siku moja nikapita maeneo ya Congo nikaona namba nikachukua, kalikuwa kabango kadogo kameandikwa "EJ COMPUTER". Nikafika home nikapiga ile namba nikajielezea kama kawaida yangu.

Basi jamaa akasema umekosea namba Mimi sio mtu wa ICT, nikamwambia namba nimechukua sehemu ni yenyewe.

Akasema nitakusaidia kitu kimoja, ila kesho pita uingalie vizuri hiyo namba.

Basi jamaa akasema ataniunganisha na jamaa yake mtu wa IT katika kampuni ya IPP MEDIA. Nilifurahi sana.

Jamaa akafanya kweli, akatokea tu kunikubali. Akaniunganisha na yule mtu na nikaenda ofisini kwao.

Nikaonana na yule mtu wa IT, nae akanikubali sana, pale pale akaniona kama ndugu yake na akaniunganisha na boss wake.

Mungu mkubwa, nikaambiwa nianze kwa kujitolea basi siku ilipofika nikaanza. Ila nilikuwa nafanya kazi sana, ile kisifa haswa kama mtu anayelipwa na nilikuwa mpole sana

Basi nilipendwa na kila mtu ikafika time nikaachiwa shift kama staff. Basi mwezi wa Kwanza tu jamaa wakaanza kunilipa mshahara. Kilichoendelea imebaki historia.

Yote kwa yote maisha yana changamoto lakini katika hizo tusiache kutumaini katika Mungu".​

20220129_151102.jpg
 
Ni mapito utakiwi kukata tamaa.

Wengine tumepita kwenye umachinga ulinzi kuwalinda watu wamelala leo tunalindwa sisi. Nilinusurika kwenda jela baaada ya lindo watu kudokoa. Nimeshiriki ujenzi wa majengo pacha BOT nikiwa kama operator wa crane za ukutani miaka 17 iliyopita.

Leo namshukuru Mungu namiliki migodi
 
Hongera sana aisee
Ni mapito utakiwi kukata tamaa.

Wengine tumepita kwenye umachinga ulinzi kuwalinda watu wamelala leo tunalindwa sisi. Nilinusurika kwenda jela baaada ya lindo watu kudokoa. Nimeshiriki ujenzi wa majengo pacha BOT nikiwa kama operator wa crane za ukutani miaka 17 iliyopita.

Leo namshukuru Mungu namiliki migodi
 
Back
Top Bottom