Stop making assumptions

ERTUGRUL BEY

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
11,534
Reaction score
21,547
Hii ni ile hali ya kuweka dhana juu ya jambo fulani au mambo fulani, kwa lugha nyingine kudhania mambo pasipo uhalisia.

Hii hali hutufanya tuishi katika ulimwengu ulio jaa uongo ndani yake,na ndio mwanzo wa matatizo,shida na changamoto nyingi ambazo tunakutana nazo katika maisha yetu ya kila siku

Mfano,unakutana na mrembo amekupa tabasamu zuri na huyo akapita zake,kitachokujia kichwani kwako ni kudhani kwamba huyu mrembo anakupenda,na utaendelea na dhana zako juu ya mahusiano yako yatakavyo kuwa,lakini kiuhalisia huyo mrembo hakupendi ila ilitokea tu akatabasamu lakini pasina hisia za mapenzi

Sasa pale unapokuja kuongea nae unagundua kwamba,hana hisia na wewe,matokeo yake unaumia moyoni,hii yote imetokana na kuweka dhana tofauti na hali halisi.

Mfano mwingine,unakutana na mtu ni mkimya sio muongeaji,sasa unaweka dhana juu yake kwamba,huyu mtu anajisikia sana au ana ringa, lakini kumbe kwakuwa hajakuzoea ndio maana anakuwa sio muongeaji,lakini baadae unakuja kugundua kumbe ni mcheshi sana kama etugrul bey

Dunia imetufundisha kudhani mambo kiasi kwamba imekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku,na wakati mwingine hatujui kama tunadhania mambo kwakuwa imekuwa sehemu ya maisha yetu.

Boss anakufokea unaanza kuweka dhana kwamba huenda hakupendi,na kibaya zaidi unaanza kumchukia kwa dhana zako,lakini kumbe ungetakiwa ujiulize kwanini inakuwa hivi,au sitimizi wajibu wangu vizuri au nimekuwa mzembe siku hizi?

Njia pekee ya kuepukana na dhana ni kuuliza maswali,hujaelewa jambo juu ya kitu fulani,basi muulize mhusika na si kuanza kuweka dhana mbaya kwa huyo mtu.

Hii dhana ndio imejikita mizizi zaidi kwa madam zetu,mkeo anaweka dhana kichwani kwake kwamba umfanyie jambo fulani,kwakuwa anadhani kwamba unamjua vizuri sana kitu ambacho si kweli. Anataka umfanyie mambo ambayo hajakwambia kwa kudhani kwamba unatakiwa ujue anahitaji nini,,yaani ni kama vile anaweka imani kwamba unajua kusoma mawazo yake.

Matokeo yake usipofanya mambo anayodhani utamfanyia,unazuka ugomvi kuwa humpendi,madam zetu wanaume nao binadamu kama nyie, kwahiyo usidhani wana kipawa cha kujua nini mnataka na nini hamtaki,mnaweza kuyafanya mambo rahisi, kwa kusema kipenz ukirudi nyumbani uje na matunda au uninunulie ile juisi yangu ninayo ipenda, huo ni mfano tu nimetoa.

Kwa yote ambayo mnahitaji waume zenu wawafanyie basi msikae kimya,waambieni na wao watafanya kwa roho safi,sasa hapo wasipo fanya ndio una haki ya kulaumu.

Tusiweke dhana juu ya mambo mbali mbali katika maisha yetu, hata katika qurani tumeambiwa hakika baadhi ya dhana ni dhambi,,chukulia kwamba umenikuta nimekaa na madam sehemu, bila hata kujiuliza mara mbili ukaweka dhana kwamba huyu ni mwanamke wangu, au nasalimiana na jirani yangu,moja kwa moja ukaweka dhana kwamba natoka na mke wa fulani,,je huoni hapo unapata dhambi?

Umenikopesha hela yako,lakini bahati mbaya,sipo vizuri kwasasa unaanza kuweka dhana kwamba nataka kukudhulumu,kitu ambacho si kweli,je umetaka kujua kwanini nimekwama kulipa kwa wakati? Ungeniuliza ningekupa majibu,,sasa kwanini unaniwekea dhana mbaya?

Ni kwa njia ya kuuliza maswali pekee ndio tutapata majibu kwa kila changamoto tunayo kutana nayo,duniani hapa kuna maswali mengi ambayo yanataka majibu, hivyo usiogope kuuliza maswali ili nyoyo zipate kutulia.

Ni hayo tu!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…