Stimulus ya Coronavirus haikwepeki kwa walalahoi na itoke Barrick Gold

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Hili gonjwa hatuna maandalizi yoyote ushauri wangu kuunusuru uchumi ni kumnusuru mlalahoi kwa kumpa kila mmoja laki moja tu aweze kujinasua na vurugu za kiuchumi zinazokuja. Mapato ya wengi yataota mbawa hivyo ni vyema tukaanza kujipanga na makamuzi yaliyopo Barrick Gold.

Hii hela ipo Barrick Gold bado hawajatulipa kile kishika mchumba au wenyewe akina Profesa Palamagamba alikiita ni "goodwill handshake" au mkono wa kheri wa dola milioni 300 USD.

Wengine walikokotoa mahesabu wakasema kila mmoja angejipatia Noah tuanze na stimulus package ya kwanza kilaki tu khalafu kama haitoshi tutarudi na awamu nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani zile michango za waathilika wa tetemeko la Ardhi kule Kagera walishalipwa?
 
wakubwa wameshachukua chao.

..tangu waanze kumchekea-chekea yule bosi wa barrick nikajua hawa tayari.
 
Laki? utaila siku ngapi ebu acheni masihara pesa ya kula siku ngapi iyo inakuwa imeisha?
 
Back
Top Bottom