Stendi ya Mwenge sasa kuhamishiwa Makumbusho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stendi ya Mwenge sasa kuhamishiwa Makumbusho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by armanisankara, Aug 23, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  Stendi ya Mabasi Mwenge


  Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam umesema kuwa wakati wowote kuanzia sasa utaihamisha stendi ya mabasi ya Mwenge na na kuipeleka Makumbusho.

  Zoezi hilo litakwenda sambamba na kuwaondoa wamachinga wanaoendesha shughuli zao za kibiashara katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria ikiwa ni pamoja na pembezoni mwa barabara na ndani ya vituo vya magari.

  Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mawasiliano wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera, wakati akizungumza na NIPASHE.

  Mhowera alisema maandalizi ya kuiondoa stendo hiyo yanaendelea na kwamba kinachosubiriwa ni kumalizika kwa zoezi la sensa litakaloanza Agosti 26, mwaka huu.

  Aliongeza kuwa matengenezo ya stendi hiyo mpya ya Makumbusho yanaendelea na kwamba hadi sasa yamekamilika kwa asilimia 75 na kuongeza kuwa kilichosababisha matengenezo hayo kuchelewa ni kuwepo kwa mgogoro kati ya manispaa na wafanyabiashara katika eneo hilo ambao kwa sasa umesuluhishwa.

  Kwa mujibu wa Mhowera, baada ya kukamilika kwa mabadiliko hayo, hakuna gari litakaloruhusiwa kuingia tena ndani kwenye stendi ya Mwenge na badala yake stendi kubwa kwa magari yote itakuwa ni Makumbusho na Mwenge litakuwa ni eneo la kushusha na kuondoka.

  Alisema zoezi hilo litaambatana na kuwaondoa wafanyabiashara wote waliokuwa wakiendesha shughuli zao kwenye stendi hiyo na nje kando kando ya barabara akisema kuwa kama walivyofanya Ubungo ndivyo itakavyokuwa kwenye eneo hilo.

  Pia aliongezakwamba wafanyabiashara wote wa bidhaa za viwandani na mashambani wanapaswa kuendesha shughuli zao kwenye masoko yanayotambuliwa kisheria na kwamba mikopo ipo kwa ajili ya wafanyabiashara watakaokubali kujiorodhesha kuhamia kwenye masoko hayo.

  Wakati huo huo, wakazi wote wa jijini Dar es Salaam katika Manispaa ya Kinondoni waishio maeneo ya mabondeni wametakiwa kuondoka mara moja kabla mamlaka haijahukua hatua yoyote ya kubomoa makazi hayo.

  Kwa mujibu wa Mhowera, zoezi hilo linahusisha pia wakazi wote ambao nyumba zao zimewekwa alama ya X na kupewa hifadhi eneo la Mabwepande nje kidodo ya Jiji la Dar es Salasaam kutokana na mafuriko yaliyolikumba jiji hilo Disemba mwaka jana na kuyarudia tena makazi hayo ya zamani.

  Aliwataka wakazi hao kuondoka kwenye maeneo hayo na kuhamia katika viuwanja walivyopewa Mabwepande.

  CHANZO: NIPASHE


   
 2. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Waongo wakubwa makumbusho washamega eneo sijui waliuza au laa, kwa kaeneo kalikobaki hakawezi kukidhi mahitaji ya kuwa stand ya mabasi yote yanayoanzia au kuishia mwenge
   
 3. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huko si ndiko walikomnanihii yule daktari? Kumbe kuna watu wanaishi huko! Hata kwa hirizi sihamii huko.
   
Loading...