Stendi mpya ya vumbi Mwanza ni kero tupu

wakozuka

Member
Mar 24, 2011
29
3
Ushauri kwa Halmashauri ya Mwanza, kwanini wasingejenga kwanza stendi iishe ndio wahamishe jamani.

Hivi mnaona hii kero iliyopo sasa? Vumbi, Usalama wakati wa usiku ni giza tu na mengine mengi tu.

Jamani angalieni hili swala tena

====

MAELEKEZO YA NAMNA YA KUFIKA ENEO LA STENDI MPYA YA MABASI YA MKOANI MWANZA

Ukiwa unatokea mjini unafika Nyegezi Corner yaani kona ya kwenda Malimbe unaendelea kama unaenda Nyegezi stend, kuna kituo cha daladala panaitwa TEMA unaenda mbele kidogo kuna bumps unavuka mpaka mbele kidogo kuna Hotel inaitwa Missana iko mkono wa kushoto.

Unaenda mbele kidogo kuna kituo cha daladala kinaitwa Kijiweni hapo ndo unashukia kabla ya kufika Kamanga Hospital angalia mkono wako wa kulia kuna barabara ya vumbi inashuka chini nenda nayo kwa chini kidogo kuna shule inaitwa Nyabulogoya unaiacha kushoto kisha unakata kulia moja kwa moja unakuwa umetazamana na hiyo stend mpya.

Kwa ufupi hiyo stend ipo katikati ya Stend ya Nyegezi na Tema Hotel au kati ya Kamanga Hospital na Tema Hotel.

Kifupi ni kwamba, unapanda gari zinazoelekea Buhongwa/Nyanshishi kama unatoka maeneo ya Mjini, Ilemela, Airport nk unashukia KIJIWENI.

Au unawaambia unashuka stand mpya ya mkoa basi.
 
Duh!! stand ipi iliohama mkuu Nyegezi ama Buzuruga na imehamia maeneo gani?

Nimetoka mwanza mwezi wa 3 sikusikia kama kuna mpango huo.
 
unaenda kidogo, unaenda tena kwa mbele,aiseeee mkuu hujui kuelekeza
 
Back
Top Bottom