Jongwe
JF-Expert Member
- Apr 25, 2008
- 1,040
- 666
Wataalam naomba kujuzwa nyumba ninayokaa ina madirisha ya zamani ya chuma kama yale ambayo watumia zaidi kule Moshi/Arusha. Kuna baadhi ya vioo vimetoka/pasuka sasa tunahangaika kubadirisha. Lakini tumeelekezwa kununua aina fulani ya putty inapatikana hapo k'koo inatwa steel putty, wanapima kwa kg. cha ajabu tumeka kwenye hizi steel frames lakini haikauki mwezi wa 3 sasa ukigusa inatoka. Tulivyo nunua tuliuliza kama inachanganywa na kitu kingine lakini jamaa muuzaji inaelekea hajui matumizi, akasema haichanganywi na kitu (ipo kama ugali laini) ndipo tulipo tumia na kutupa hayo matoke. Je wataalam mnajua hii kitu inachanganywa nini?