kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,527
- 17,643
StarTimes ile kampuni inayorusha matangazo ya television kwa njia ya ving'amuzi (digital) kwa ubia na TBC inaonekana sio rafiki kwa vijana wa taifa hili, Inajulikana vijana wa nchi hii ni washabiki wa kutupwa wa soccer, hebu ona StarTimes na TBC inashindwa kuwa na channel ya kuonyesha hata mashindano ya finali mbalimbali za kabumbu nchini, Afrika mashariki, Africa, Ulaya na hata kombe la dunia. Huku ni kuwakosea adabu vijana na wapenda mpira wa miguu nchini.
Ni kawaida kuona television za KBC na UBC zikionyesha mashindano ya kombe fulani kwa wananchi wao lakini sio TBC, TBC haijali vijana wake wanaolazimika kutafuta vituo vya supersport ili kutimiza haja zao za kuangalia mashindano mbalimbali. bahati mbaya vijana hawa (wadogo) wako tayari kungojea muda wa kuanza mpira husika hata ikibidi usiku wa manane wakati wazazi wakiwa wameshalala majumbani mwao.
Bahati mbaya nyingi ya television hizi huwa ziko maeneo yanayouza pombe (bar) kitendo kinachowafanya watoto wachanganike na walevi wenye matusi mazito, vijana huwa wanaumwa na mbu usiku kucha kitendo kinachochangia kupata homa za malaria zinazowafanya wasihudhurie shule na masomo vema. Pia vijana hawa huwa wanalazimishwa kulipa kiingilio ama kununua vinywaji (soda, maji, juice) kwa bei ya juu ili kuhalalika kuangalia mpira.
Tabia hii ya kulipia inawafanya vijana wawe wadokozi ili kupata hela ya kumuona Messi na Rolnado kwa gharama yoyote.
StarTimes na TBC waoneeni huruma watoto wetu angalau kwa ving'amuzi walivyonavyo majumbani mwao waweze kuangalia mashindano mbalimbali ya mpira japo kwa ada ya sh. 10,000 kwa mwezi. TBC inaendeshwa na kodi za wazazi wao, hivyo kuwaonyesha watoto mpira wakiwa majumbani mwao ni sehemu ya huduma hata kama kufanya hivyo ni ghali. Hii itasaidia kuwajenga vijana badala ya kurandaranda usiku wa manane kwenye mabaa,
Hatari iliyoko sasa watoto na vijana wameshaaza kuichukia StarTimes na TBC1, wanawashauri wazazi wao warudishe ving'amuzi vya Startimes maana havina maana kwao