Stars kuanza kusaka heshima leo

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
TIMU ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo inaanza kutupa karata yake ya kwanza katika mashindano ya nchi za Ukanda wa Bonde la mto Nile na Ziwa Victoria Nile Basin , itakapovaana na Burundi Indamba Murugamba , kwenye Uwanja Taifa mjini Cairo, Misri.
Stars inayonolewa na Mdenish Jan Poulsen ambaye aliungana na timu hiyo juzi majira ya saa 8 usiku, inavaana na Burundi ikiwa na kumbukumbu ya kuilaza mabao 2-0 wakati wa mashindano ya CECAFA Chalenji hivi karibuni jijini Dar es Salaam, yote yakipachikwa na Nurdini Bakari.

Katika hatua nyingine, nyota wawili wa Stars Rashid Gumbo na Athumani Machupa wanatarajiwa kukwea pipa leo kwenda jijini Cairo Misri kuungana na wenzao.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni, wachezaji hao, daktari wa timu na viongozi watatu walikwama kuondoka juzi baada ya kutokea mkanganyiko wa majina katika tiketi zao.

Alisema, tiketi zilizokuwa zimetumwa zilikuwa zimechanganywa majina kwa wachezaji na viongozi hao hivyo kutofautiana na majina yaliyomo katika pasi zao za kusafiria, hali iliyoleta mkanganyiko na TFF kulazimika kuwasiliana na Shirikisho la Soka nchini Misri ili kuzifanyia marekebisho.

Aliwataja viongozi wanaondoka na timu hiyo ni aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa TFF, Cresentius Magori, Idd Mshangama, Merrey Balabhou na dakari wa timu hiyo Dk. Nandi Mwankemwa.

Wakati Stars ikianza kampeni hiyo jioni, timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars mchana itakuwa na kibarua kigumu kwa kukumbuna na Sudan.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom