mimi nafikiri watanzania tunamatamanio na ndoto kubwa sana, naelewa kua kutamani na kuota ndoto chanya sio dhambi wala sio tatizo.
ila unapo ota na kutamani zaidi ya uwezo wako ni tatizo, watanzania wanalaumu matokeo ya taifa stars na mchakato mzima wa uendeshaji timu kwa ujumla utafikiri timu ilikua inashinda vikombe na kufanya vizuri hapo awali kabla ya kuja maximo.
tumejisahau ya kua mpira wa miguu au jambo lolote lile iliuwe na mafanikio unaitaji matayarisho ya muda mrefu sana na kijipanga kwa mipango inayo tekelezeka na kueleweka kwa watendaji wenye nia ya kutekeleza.