eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,235
- 16,205
Alizaliwa 23/10/1940 mjini minas na kukulia katika mji wa sao paulo
Alianza soka ya kulipwa katika klabu ya santos akiwa na miaka 15
Aliitwa timu ya taifa ya brazili akiwa na miaka 17 tu katika fainali za kombe la dunia nchini sweeden
Alianza kufanya maajabu katika fainali hizo kwa kufunga bao akiwa na umri mdogo na kuweka rekodi ambayo haijavunjwa mpaka leo
Pia aliisaidia brazili kutwaa kombe hilo akiwa na umri wa miaka 17 tu huku akifunga mabao mawili katika final dhidi ya sweeden katika ushindi wa bao 5-1
Ni mshindi mara 3 wa kombe la dunia 1958 1962 1970
Alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa kombe la dunia mwaka 1970
Alicheza finaly 4 za kombe la dunia 1958 1962 1966 1970
Pele ni mchezaji wa kwanza kufunga bao la 1000
Alichezea santos karibu maisha yake yote lakini alikwenda marekani katika club ya new york cosmos ambayo aliichezea kwa miaka 3 kabla hajatundika daluga
Alicheza mechi 1365 katika maisha yake yote ya mpira
Na katika mechi hizo alifunga magoli 1280
Idadi ambayo haijafikiwa na mchezaji yeyote hadi sasa
Pia huyu ni bingwa wa kukokota mpira duniani bila kuchukuliwa na mpinzani wake
Yapo mengi lakini haya ni machache kuhusu mfalme wa kandanda duniani kwa muda wote