Nimekuwa nikiifuatilia star TV vipindi vya mijadala ya asubuhi, kwa ujumla mijadala wanayoweka ni mizuri lakini tatizo liko kwenye utoaji nafasi kwa wazungumzaji, akiwepo mzungumzaji ambaye mlengo wake ni kutetea serikali au ccm anapewa nafasi kubwa na wakati mwingine huyo mtu anaongea maneno ya jumla jumla tu anaenda porini wanamuacha.
Akiwepo mpinzani au mwenye maoni tofauti huyo mtu anapewa nafasi kidogo na wakati mwingine anakatishwa au ananyamazishwa asitoe nondo zake. Mfano ni leo asubuhi kijana wa chadema alitaka kuelezea political stability inavyoweza kuathiri uchumi yule kijana alinyamazishwa asiongee kuhusu hilo. Tutakuwa tunajidanganya kwamba uchumi unaweza kukua bila kuwa na uthabiti wa kisiasa.
Kwa hiyo Star TV najua mnaweza mkawa mnapata shinikizo ukizingatia Diallo ni CCM damu damu lkn kama mnaamua kujadili jambo waache watu waongee.
Nawakilisha wadau