Sura huwa hainipi matatizo kinachonipa matatizo kinachosemwa na mleta habari...mleta habari huyo umsemaye alipata aibu ya mwaka kwa kusema sema hovyo kwa mtindo wa mashabi wa kibongo bongo, enzi za Maximo wa Taifa Stars. Kipindi hicho Maximo alikuwa ameshikia kidedea nidhani ya wachezaji ndani ya timu...kutokana na nidhamu mbovu ya wachezaji wazoefu, Maximo aliamua kuwatema na kuchukuwa wachezaji wasio na majina na kuipeleka timu kwenye pambano la kiushidani huko Africa magharibi (nchi sikumbuki vizuri ni hipi).
Basi huku nyuma mleta habari huyo...aanza kumkashfu na kumkebehi Maximo kupitia vipindi vya michezo vya Star TV kwa kushirikiana na watangazaji na waandishi makanjanja wa habari za Michezo.....Kikosi cha maximo kilishida mechi ya Ugenini 1-0 nina kumbuka vizuri sana .....kwa aibu kubwa Star TV hawakumpa jukwaa tena kwenye masuala ya michezo karibu miezi sita.