Stanslaus Mabula akabidhi vitabu vya shilingi milioni 12 shule ya sekondari Mkuyuni

Jemmie

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
216
285
Mhe Stanislaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana kwa ushirikiano wa ufadhiri wa taasis ya SOS amekabidhi vitabu 452 vya Sayansi pamoja na masomo yenye michepuo ya Art na uchumi katika shule ya sekondari Mkuyuni vyenye thamani ya shilingi 12,000,000. Vitabu hivyo ni msaada kutoka taasis hiyo ili kuimalisha sekta ya elimu Wilayani Nyamagana. *Nawapongeza wadau wa maendeleo SOS kutoa vitabu 452 shule ya sekondari Mkuyuni msaada unaowezesha utekelezaji wa Sera ya elimu ya Mwanafunzi mmoja Kitabu kimoja* Mhe Mabula amesema

Hafla hiyo imefanyika katika ziara maalum ya Mbunge Jimbo la Nyamagana katika taasis ya SOS akiambatana na viongozi wa SOS wakiongozwa na Kaimu Maneja Ndg. Samson, Mhe . Donator Yusuph Gappi Diwani mwenyeji, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kata Mhe. Baluani watendaji wa Serikali Kata na mitaa Mkuyuni pamoja na ujumbe wa Taasis ya First Community Organization.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana
 
Yani uyo Jamaa ni boya sana jiji kama mwanza linahitaji mbunge machachali afadhali ya msukuma au kibajaji lkn all in all Ccm hapa hawatakiwi
 
Back
Top Bottom