Standards za majengo Kariakoo ziboreshwe, panatia aibu!

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,889
43,779
Jana nilipita Kariakoo kwenye makutano ya barabara ya uhuru na msimbazi (ilipokuwa round about) na kukuta kuna jengo la NHC linavunjwa, naamini ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya (au renovation).
Sasa naomba nijibiwe maswali haya na watu wa manispaa. Kama hampokei rushwa:-

1.) Ni kwanini mnaruhusu mtu anajenga jengo la ghorofa kumi bila kuonyesha kwenye michoro yake kwamba hizo familia almost 20, maduka almost 10, na wateja wao watapaki wapi magari?! Hizo building permit huwa wanazipataje pataje kama sio hongo na rushwa?

Nyinyi ndio mnasababisha kariakoo inakuwa kama banda la kuku au zizi la ng'ombe, its total chaos! Magari tupaki wapi?! Mbona kule posta majengo yanayojengwa siku hizi yanakuwa na either underground parking, 1st & 2nd floor parking, au jengo maalum la parking pembeni. Majibu Tafadhali!

2.) Ni kwanini mnaruhusu majengo mawili marefu kubabanana kama abiria wa daladala wakati sheria za setbacks zinahitaji kiwango maalum cha kuachana baina ya jengo moja hadi lingine ili kuwezesha upumuaji mzuri wa majengo, kwani kwenye michoro yao huwa hawaonyeshi setbacks? Wanapata vipi hizo building permit? Majibu tafadhali!

Kama hilo jengo la NHC linalovunjwa pale uhuru/msimbazi ni kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya, nitahakikisha mnafanya yafuatayo, mnaweka parking space either underground au above ground kwa ajili ya magari ya watumiaji wa jengo husika, kinyume cha hapo tutaaibishana humu, kwani nitaweka updates humu ya hatua kwa hatua ya jinsi jengo lililopewa building permit linakosa provision za parking katikati ya jiji.

Nitaweka picha za hatua kwa hatua za ujenzi, nitaweka building permit no., jina la client, jina la Architect aliye-design huo uozo, jina la structral eng., Quantity Surveyor na sub-contractors wote watakao kuwa wanajenga huo utumbo

Hali ya kukosa parking kwa kweli inaleta a very stressful and chaotic environment kwa madereva wanaolazimika kupaki barabarani na bado wanalipa 5,000/= kwa siku!
 
Back
Top Bottom