Stahili ya Uhamisho wa Watumishi wa Halmshauri ya Wilaya

Suip

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,338
803
Wataalam wa humu JF naomba
kufahamishwa Stahili ya Mtumishi
yeyote wa Halmashauri je
anapohamishwa kituo cha kazi ndani
ya Halmashauri husika, anastahili
kulipwaje kwa Ngazi ya Mshahara
wa TGHS B mathalan analipwa Tsh
562,000/=?
Kwani hakuna uwazi kwa malipo
utakuta mtumishi kahamishwa toka
Mwaka 2013 mpaka leo hajalipwa
anadai tu na hajui anadai kiasi gani.
Kwa anayefahamu tafadhali asaidie
na kanuni inasemaje kwani Maafisa
Utumishi wengi hawako wazi na
watumishi wengi wa ngazi ya chini
wananyanyasika.
 
Mi nijuavyo...Ukiwa mfanyakazi wa halmashaur husika,Ina maana wewe ni unaweza kutumika katika kituo chochote ndani ya Hiyo Halmashaur....na Tena najua hata kitambulisho chako kitaonyesha kuwa wewe ni mtumishi wa hiyo Halmashauri katika Cheo fulan, na hicho kitambulisho hakitasema ni kituo gani unafanyia kazi....

So,kulingana na uelewa wangu,Ndani ya Halimashauri haulipwi....labda kutoka Halmashaur moja kwenda nyingine au Mkoa.
 
Kwa uelewa wako sawa lakini naamini haiwezekani mtumishi kuhamishwa umbali wa km60 kutoka kituo cha mwanzo kwenda kingine bila kulipwa usafirishaji wa mizigo yake na posho ya kujikimu na ya usumbufu.Lazima Kuna malipo ila Maafisa wa Halmashauri wengi wanaohusika na malipo hawaweki malipo hayo wazi.
 
Stahili ya uhamisho inategemea kama mhusika amehama makazi (physical transfer).mfano kama umetoka shule A kwenda shule B ya karibu haina malipo. Ila kama umehama na makazi kutokana na umbali utalipwa posho ya usmbufu ambayo ni asilimia 10 ya mshahara wa mwaka+gharama za kusafirisha mizigo+nauli ya (mtumishi, mwenza na watoto/wategemezi wasiozidi wanne)+posho ya kujikimu ya siku 14 kwa waliotajwa hapo awali bali wategemezi hulipwa nusu inategeme na ngazi ya mshahara.
 
Napata mwanga ila naomba ufafanuzi ni siku 14 au 7?
 
Siku 14 uhamisho siyo siku saba.
Shukran kwa maelezo yako, Posho ya usumbufu umeeleza ni 10% ya mshahara wa mwaka ila hiyo posho ya kujikimu ya siku 14 inakokotolewa kwa vigezo vipi?
 
Back
Top Bottom