Stade des Martyrs, Congo: AS Vita Club 5 - 0 Simba SC

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Leo tunashuka dimbani kucheza mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club.

IMG_20190119_190337.jpg

Kikosi cha akiba cha Simba
1. Deogratius Munish
2.Paul Bukaba
3.Moahamed Ibrahim
4.Haruna Niyonzima
5. Hassan Dilunga
6. Rashid Juma
7. Shiza Kichuya

Hiki ndio kikosi cha mauaji kitakachoshuka dimbani leo kufanya mauaji

========


Timu ya Simba imepoteza mchezo wake wa pili hatua ya makundi baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya AS Vita.

Mabao ya mapema ya AS Vita yaliwekwa dakika ya Makusi 14' Bpunga 18 na Fabrice Ngoma 45 kipindi cha kwanza.

Mabao mawili ya AS Vita yaliwekwa wavuni kipindi cha pili huku wakionekana kulifikia lango la Simba mara kwa mara.

Mchezo huo ulionekana mkali huku Paschal Wawa na Jonas Mkude wakipewa kadi za njano.

Kocha wa Simba Patrick Aussems alimtoa Cleoutus Chama na nafasi yake kuchukuliwa na Dilunga dakika ya 61.

Katika Kundi D, AS Vita ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 3 huku ikifuatiwa na Simba yenye alama 3 ikizidiwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Baada ya mechi ya AS Vita vs Simba kumalizika, nilikutana na kocha msaidizi wa Vita Raoul Shungu ambaye si mgeni kwa watanzania kwa sababu aliwahi kufundisha Yanga.

Shungu amezungumzia mambo mengi kuhusu mchezo wao dhidi ya Simba, amesema kuwa waliangalia mechi kadhaa za Simba na kubaini mapungufu ambayo wameyatumia na kupata ushindi.

“Simba ni timu nzuri lakini wanacheza mpira ambao sio wa kasi, wanapiga pasi ambazo kwenye mashindano hazina faida, wanapoteza muda mwingi kupiga pasi za hapa na pale badala ya kwenda mbele kutafuta nafasi. Sisi tunarudi nyuma tukipata mpira tunacheza kwa speed.”

Shungu amesema katika kipindi chote alichofundiaha Yanga, alishinda mechi zote alizokutana na Simba.
 
Back
Top Bottom