RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kuzingatia mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza baada ya kuunda Kamati hizo mwezi Januari 2016. Mabadiliko hayo, yamefanywa chini ya Kanuni yo 116(3) yo Kanuni za Kudumu za Bunge inayompa Mamlaka ya kuteua Wabunge kuunda Kamati Mbalimbali za Bunge.
Aidha kufuatia mabadiliko hayo ambayo baadhi yake yamehusu Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au wote wawili, Kamati za Kudumu za Bunge zilizoathirika na mabadiliko haya zitawajibika kufanya Uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa kanuni yo 116 (10) kama ifuatavyo:
1. Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii inahitaji kupata Mwenyekili na Makamu Mwenyekiti wapya.
2. Kamati ya Nishati na Madini itahitaji kupata Mwenyekiti mpya.
3. Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma itahitaji kupata Mwenyekiti mpya.
4. Kamati ya LAAC itahitaji kupata Makamu Mwenyekili mpya.
5. Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya.
Mabadiliko haya kwenye kamati zote yanaanza mara moja ambapo orodha ya wajumbe waliobadilishwa imeambatanishwa.
lmetolewa no:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
22 Machi, 2016.