Spika si yule, CCM si ile na CHADEMA si ile NCCR wala CUF

Django

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
354
147
MWENENDO wa mijadala katika Bunge la Bajeti linaloendelea huko Dodoma una mengi ya kutufundisha.

Kwa sababu zisizojulikana wazi, kila inapotokea Naibu Spika Job Ndugai akawa zamu, joto huwa linapanda na kusababisha itikadi kutawala badala ya hoja zenye maslahi kwa Taifa. Vitendo vya kuwatoa nje wabunge wa upinzani vimetokea chini ya uongozi wa Job Ndugai na kuacha makovu makubwa katika heshima ya Bunge letu.

Joto la mijadala bungeni limesababisha baadhi ya watendaji wa serikali na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kuja na utabiri juu ya hatima ya upinzani hapa nchini.

Watabiri hao wakiongozwa na Stephen Wassira, Mwigulu Nchemba, Job Ndugai na Nape Nnauye wamedai kwa nyakati tofauti kuwa CHADEMA hakina lolote na kitasambaratika kama kilivyosambaratika NCCR-Mageuzi, TLP na CUF.

Wanadai kuwa vyama hivyo viliongoza upinzani wa kweli bungeni na viliheshimu kanuni na taratibu za Bunge na hoja zao zilikuwa za kistaarabu. Wanaendelea kusema, chini ya CUF kama kambi rasmi ya upinzani bungeni, hoja zenye maslahi ziliwasilishwa na serikali sikivu ilizifanyia kazi bila mabishano kama ilivyo sasa.

Watendaji hawa na makada wa CCM wanajenga hoja kuwa CHADEMA kitasambaratika kabla ya mwaka 2015. Kabla sijajielekeza katika kuchambua madai haya nibainishe mapema udhaifu wa madai haya ya CCM dhidi ya upinzani.

Hoja hii ni dhaifu kwa sababu pamoja na unaodaiwa ni uzalendo na ustaarabu wa NCCR-Mageuzi, TLP na CUF ndani ya Bunge, bado makada hao hao wa CCM wanakubali kuwa vyama hivyo ama vimesambaratika au vimepoteza mvuto mbele ya Watanzania. Kigezo cha kupungua kwa mvuto wa vyama hivyo ni ukweli kuwa vyama hivyo vimepoteza viti vingi bungeni na viti vya madiwani katika halmashauri mbalimbali nchini.

Kwamba, pamoja na kusifiwa na CCM kuwa vyama hivyo vilikuwa vinafuata kanuni vizuri ndani ya Bunge na kuwa vilijenga hoja nzuri na zenye maslahi kwa Taifa, bado CCM wanakubali kuwa vyama hivyo hivi sasa vimepungua nguvu yake katika medani za kisiasa.

Hii ina maana kuwa kusifiwa na CCM ukiwa mpinzani si mtaji wa kujivunia bali sifa wanazomimina CCM ni tangazo la ushindi dhidi ya wapinzani. Wapinzani wote wa kweli inawapasa kushtukia sifa hizi wanazomwagiwa na serikali. Sasa turejee katika mada ya wiki hii.

Kuna mabadiliko makubwa bungeni. Yanaweza kuwa mabadiliko hasi na chanya pia. Sehemu zote tatu, yaani Kiti cha Spika, CCM na Upinzani vimekumbwa na mabadiliko makubwa ndani ya Bunge. Hata ukiichambua CCM yenyewe ndani ya Bunge yaani wabunge, Serikali na hata Kiongozi wa Shughuli za Serikali ndani ya Bunge, kuna mabadiliko makubwa.

CCM iliyokuwa inanyukana na NCCR-Mageuzi kuanzia mwaka 1995, au TLP miaka iliyofuata ni tofauti na CCM hii ya sasa. Kadhalika, CCM iliyonyukana na CUF kikiwa chama kikuu cha upinzani bungeni ni tofauti na CCM ya sasa. CCM ile ilikuwa bado na chembechembe za uzalendo na kujali maslahi ya Taifa. CCM ile ilikuwa na chembechembe za uthubutu wa kushughulikia kero za wananchi kama rushwa, ufisadi, kutowajibika na hata kukusanya kodi.

CCM ile ilikuwa na jeuri ya kuwawajibisha watendaji wa serikali na hata kuwahoji bila kujali tuhuma dhidi yao zimetolewa na nani. CCM ile ilikuwa na ujasiri wa kukubali kuwa ilani yake ya uchaguzi si halisi (realistic).

Hii ina maana CCM ile ilikuwa na uwezo wa kukubali makosa na kujikosoa kama njia ya kujipanga upya. CCM ile ilikuwa na jeuri mbele ya matajiri hata kama walikuwa wanaifadhili. Baadhi yao iliwafuta katika vinyanganyiro kadhaa pale walipogombea nafasi mbalimbali ndani ya chama.

CCM ile haikuona fahari katika kuombaomba kwa wafadhili kama njia ya kuleta maendeleo kwa Taifa. CCM ile ilisisitiza, mara kadhaa, kuwa maendeleo yatakuja kwa njia ya kujitegemea, si kutembea na bakuli dunia nzima kuomba misaada.

CCM ile ilikuwa na wabunge waliokuwa wakichangia ndani ya Bunge wakipendekeza njia mpya za kupata mapato kwa kuanzisha vyanzo vipya.

Ya leo ni tofauti. CCM ya sasa inaibana Serikali ili ifute vyanzo vya mapato ili vigogo wapate uchochoro wa kufanya biashara bila kulipa kodi. Kwa hiyo kimsingi nisisitize kuwa CCM ile iliyopambana na wapinzani kama NCCR na CUF na kuweza kuwashinda, haipo tena. CCM ile ilisambaratika sambamba na kusambaratika kwa vyama vya upinzani vya wakati huo.

CHADEMA ndicho chama kikuu cha upinzani kwa wakati huu. Kimelaumiwa na kulaaniwa na watawala pamoja na makada wa CCM kuwa ni chama cha kigaidi, cha kikabila, cha kidini, kisicho na uzalendo, kisichojua Kanuni za Bunge, cha msimu, cha kiana harakati, na sifa nyingine mbaya mbaya. CHADEMA hiki kinacholinganishwa na NCCR, TLP na CUF ya wakati ule, hakionekani kuwa na dalili za mfanano huu. Nifafanue kidogo.

CHADEMA hii inasoma makabrasha hata kama inadaiwa haina wabunge wasomi. Watazamaji wa mijadala ya wabunge wameshuhudia wabunge wa CHADEMA wakiibua makosa makubwa katika makabrasha ya Serikali.

Tabia hii ya wabunge wa CHADEMA imelisaidia Taifa kujua kuwa kuna uzembe wa watawala katika kuwasilisha mijadala bungeni. Si siri kuwa hivi sasa mawaziri inabidi wajipange kabla ya kuwasilisha hoja zao, maana wana uhakika kuwa wabunge wa CHADEMA wanasoma makabrasha yao.

CHADEMA hii inasoma na kufuata Kanuni za Bunge hata kama inalaumiwa kuwa haifuati kanuni. Kwa macho ya watazamaji, tumeshuhudia Bunge likilazimika kufanya marekebisho ya kanuni ili kuwabana zaidi wabunge wa CHADEMA.

Ili kuinusuru Serikali na hoja za wapinzani, Bunge hili lililazimisha kubadili kanuni ili kupunguza nguvu ya wapinzani bungeni pale kanuni zilipotambua uwepo wa kambi rasmi ya upinzani na isiyo rasmi bungeni.

Lengo la kanuni hii ilikuwa ni kuwagawa wapinzani bungeni ili iwe rahisi kuwatawala. Matokeo yameonekana kwani wapinzani wengine nje ya CHADEMA, wanalazimika kuiunga mkono Serikali kuliko hata inavyoungwa mkono na wabunge wa CCM.

Kadhalika, Spika huyu ni tofauti na maspika wengine waliotangulia. Tunakumbuka Adam Sapi Mkwawa, Pius Msekwa na Samwel Sitta. Wote walipokaa katika kiti cha Uspika, walisahau wanatoka chama gani na tuliwaona daima wakikumbuka wanatoka Taifa gani. Walionekana daima kama majaji waliovaa haki na ukweli.

Ndiyo maana kuna baadhi ya wana CCM wanaodiriki kusema Bunge la Chama Kimoja lilikuwa na upinzani wa kweli kuliko la sasa lenye vyama vingi.

Wanasema haya wakimaanisha kuwa chini ya maspika hao, maslahi ya Taifa yalipewa nafasi na wananchi walitetewa kwa upana wake. Chini ya Spika huyu, maslahi ya Taifa yamefunikwa na maslahi ya chama tawala na watawala.

Haishangazi kuona Spika akiungana na wabunge wa CCM kuzuia maswali, hoja binafsi zenye maslahi na hata kuzuia ripoti za tume zisisomwe bungeni.

Kimsingi, mambo mengi yamebadilika na kwa hiyo si sahihi kudai kuwa CHADEMA itasambaratika kwa kuwa tu, hata NCCR, TLP na CUF vimesambaratika ndani ya Bunge. Msambaratiko umetokea pande zote kama nilivyojadili.

Mwenendo wa siasa nchini unaonyesha dhahiri kuwa umeshuka kwa ubora na idadi. Kwa mtazamo wa wengi, CHADEMA imesadia sana kuwaonyesha wananchi ni wapi kuna uzembe na udhaifu katika uendeshaji wa serikali.
 
CHADEMA sumu ileile,ugaidi uleule.maandamano yaleyale,migomo ileile,udini uleule,ukabila uleule,ukaskazini uleule.uazinzi uleule.r.i.p CHADEMA
 
Mwenendo wa siasa nchini umaonyesha dhahiri kuwa umeshuka kwa ubora na idadi.

Huu ndio ukweli, hii ndio hali inayodhihirishwa na Bunge - kutetea tu ili mradi alitoa hoja sio wa upande wetu.
 
chadema sumu ileile,ugaidi uleule.maandamano yaleyale,migomo ileile,udini uleule,ukabila uleule,ukaskazini uleule.uazinzi uleule.r.i.p chadema

CHADEMA moto uleule wa kuwawakilisha wananchi bungeni ipasavyo wewe na wenzako mnaumwa ugonjwa unaitwa CHADEMA-phobia hadi uje ukutoke huo ugonjwa inabidi ukubali mabadiliko utaumwa sana huo ugonjwa,haya nenda kachukue bukusaba zako Lumumba wahi foleni hii.
 
Back
Top Bottom