Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,883
Ndo maneno ya Ndugai mbele ya kamera za Azam tv.
Na anasema inamaana wagombea kwanini ni wakristo tu, kwanini hakuna wazanzibari, kwanini wateuwe watu toka jimbo moja tu la Nyamagana, kwanini hakuna wanawake
Na anasema inamaana wagombea kwanini ni wakristo tu, kwanini hakuna wazanzibari, kwanini wateuwe watu toka jimbo moja tu la Nyamagana, kwanini hakuna wanawake
SPIKA NDUGAI. Kama CHADEMA wataendelea kuchezea hiyo nafasi tutawapa vyama vingine vya upinzani. Spika Ndugai akiongea na Azam Tv amesema CHADEMA wamepewa nafasi ya mwisho.
Kama wataichezea kwa kuleta wagombea waliokataliwa basi hizo nafasi mbili watapewa vyama vingine vya upinzani,kama ACT na NCCR.
Spika ameongeza kwa kusema kuwa nafasi hizo mbili za ubunge wa Afrika Mashariki hazipo kisheria. Amesema nafasi hizo yeye ndiye alitumia kanuni tu za bunge kuwapa nafasi mbili CHADEMA.
Anaweza akabadili kanuni na kutoa nafasi kwa vyama vingine.Kuhusu CHADEMA kwenda mahakama Spika Ndugai amesema yeye hawakatazi kwenda huko ila lazima wajue kuwa mahakama na bunge ni Mihimili miwili inayojitegemea.
Katika hatua nyingine Spika Ndugai ameshangazwa na uamuzi wa CHADEMA kuchagua wagombea wa ubunge wa Afrika Mashariki huku wote wawili wakitokea jimbo moja la Nyamagana na pia wote wakiwa wa jinsia moja na imani ya aina moja wakati chama kina maelfu ya wanachama wa kila aina.
Chanzo: Azam TV