SPIKA NDUGAI CAG AMEKUSHIKA PABAYA.

Mra Eliphas

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2017
Posts
264
Reaction score
235
Spika Ndugai umesikika tena ukitamba eti CAG prof. Assad asipotii amri yako batili ya kwenda mbele ya kamati ya maadili ya bunge, utamshangaza.

Utamshangaza kwa lipi? Huna uwezo wa kumfunga jela kutokana na jinai yoyote aliyotenda, huwezi kumpiga fimbo kama ulivyompiga yule mshindani wako ccm, na hata ukimchongea kwa swahiba wako amuondoe kwenye nafasi hiyo, bado profesa hana shida na ajira , maana huyu anaweza kuajiriwa popote duniani tena na mshahara mnono kuliko alio nao sasa .
Na sana sana ukila njama na kuendelea kuvunja katiba kwa CAG kufungwa pingu kama unavyotamba, bado profesa atatoka lockup ndani ya muda mfupi na hapo ndio utakuwa umejipalia mkaa dunia kujua uovu wako wa kuvunja katiba ya nchi yetu kwa maslahi ya ccm.

Kimsingi prof. alishakujibu, kwamba fuata katiba na siyo amri zako, ibara ya 18(a), (b). ibara 26(1),(2) Na ibara 143.

Ndugai wewe ndiye utatoka knocked out kama utaendelea na mpango wako wa kumdhalilisha CAG kwa kuwa amesema ukweli kwamba bunge ni dhaifu.

Hivi uwanja wa ndege wa Chato kujengwa kwa mabilioni, bila idhini ya bunge siyo udhaifu wa bunge huo? Hivi ndege za mabilioni kununuliwa bila idhini ya bunge siyo udhaifu wa bunge huo? Hivi hadi leo 1.5 trillions kutokutolewa maelezo na serikali zilikwenda wapi siyo udhaifu wa bunge huo? Spika Ndugai Wacha kukurupuka kwa maslahi ya ccm, tetea maslahi ya taifa kama CAG, siyo ccm.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watanzania bado ni shida na kwa staili hii tusitegemee maendeleo.
 
Kuna uwezekano Ndugai hajui wajibu wa spika. Anadhani ni kumnyamazisha Heche na Bulaya na kiboko yake Halima Mdee. Ndugai. You may consult mama Makinda. Hii itakusaidia hata nyumbani kwako kifamilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…