Spika Ndugai anatibiwa India

Spika Ndugai anatibiwa India

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai yuko nchini India kwa matibabu ingawa haijulikani yuko hospitali gani na kwa muda gani sasa. Katibu wa Bunge, Dr. Thomas Kashililah amesema kuwa Spika Ndugai amekwenda nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake bila ya kusema amekwenda nchi gani wala ugonjwa unaomsumbua. Amesema kuwa Spika haumwi sana.

Lakini Balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi amekiri kuwa Spika Ndugai uko India kwa matibabu na anaendelea vizuri. Kimsingi, Ofisi ya Bunge imedai kuwa Spika yuko nje ya nchi kwa uchunguzi wa kiafya wakati Ubalozi umesema kuwa Spika yuko India kwa matibabu.

Chanzo: Mwananchi la leo, uk. 3

 
Asante kwa taarifa japo zinakinzana kidogo. usjali kuhusu bunge maana yuko Naibu wake, kiubinadam tu tumwombee arudi salama aendele na huu mziki wa Bongobunge.
 
Kwani tanzania hakuna madaktari na hospitali hadi aende kutibiwa india. Hii inaleta picha gani kwa wananchi wa kawaida
 
Sioni kipya hapo, zaidi ya kujaza server tu kwa "odd data"
 
Kwani tanzania hakuna madaktari na hospitali hadi aende kutibiwa india. Hii inaleta picha gani kwa wananchi wa kawaida

Ina maana alipata kibali cha kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi? Kazi kweli kweli
 
Mbona tuliambiwa hakuna kutibiwa nje?
 
Anatibiwa kwa hela zetu uyu waseme wameenda tibiwa nini ili tupime uzito wa tatizo
 
Hii imekuwa nchi ya watu watatu i.e Rais, Spika wa bange, na Jaji mkuu.

Kwa kisingizio cha kubana matumizi.

Sisi kwa utanzania wetu unaofanana na wa kwao tunatibiwa kwa dokta Mwaka

MIMI SIMUOMBEI APONE, KWA MAANA YEYE AKIPONA KUNA WATAKAOKUFA BADALA YAKE. JIOMBEE USIWE WEWE ANGALAU KWA SASA.
 
Kwani tanzania hakuna madaktari na hospitali hadi aende kutibiwa india. Hii inaleta picha gani kwa wananchi wa kawaida
Yaani hilo ndo swali langu siku zote; tatizo ni kwamba madactari wetu hawana viwango au ni tatizo la vifaatiba. Mi natumaini kuwa itafika siku katika hii awamu ya tano, hawa miungu watu wataacha kwenda kutibiwa nje kwa gharama kubwa ya walipa kodi. Hebu Mungu amjaze raisi wetu hekima na utashi; mawaziri wajawe na hofu ya Mungu wafanye kazi kwa weledi na kuweka mipango endelevu ya kuondoa kabisa huu utegemezi. Tumechoka!!
 
Tutaweza kubana matumizi kweli? Haya uguwa pole mh.supikaa
 
Safari za nje zimepigwa stop kwanini Ndugai kasafiri aua anasubiriwa akirejea asimamishwe kazi.
 
Back
Top Bottom