Spika Ndugai afanya tena mabadiliko ya Kamati za Kudumu za Bunge

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko mengine ya kamati za Bunge kwa kuwaongeza wabunge wapya na kuwahamisha wengine kwenda kwenye kamati nyingine, jambo ambalo limepingwa na baadhi ya wabunge wakidai linapunguza ufanisi.

Juzi, Spika Ndugai aliwaongeza wabunge wanne wapya walioapishwa bungeni Aprili 19, kwenye kamati za Miundombinu; Ardhi, Maliasili na Utalii; Kilimo, Mifugo na Maji; na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Hayo ni mabadiliko ya pili tangu Bunge la 11 lianze rasmi vikao vyake katikati ya Novemba mwaka jana, ikiwa ni kipindi kifupi cha mabadiliko ikilinganishwa na Bunge la Tisa na 10.

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Bunge, mabadiliko hayo yamefanyika kwa mujibu wa kanuni ya 116 (3) na (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2016, ili kuhakikisha kila mbunge anakuwa mjumbe wa kamati mojawapo ya Bunge. “Aidha, mabadiliko haya ni kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kadri itakavyowezekana, Muundo wa Kamati za Kudumu za Bunge unazingatia aina za wabunge kwa jinsia, pande za Muungano na Vyama vya Siasa vyenye uwakilishi bungeni, ujuzi maalumu, idadi ya wajumbe kwa kila kamati na matakwa ya wabunge wenyewe,” inasema taarifa hiyo.

Wabunge wampinga Ndugai kubadili kamati
 
Huyu spika wa sasa afadhali hata mama Makinda
Na kwa kweli hata afya ya Job naona kama si nzuri hivi,si mchangamfu kama wakati uliopita,sura imepoteza nuru na bashasha...Inawezekana ikawa sbb ya yeye kuwa inactive katika mambo yake
 
Wewe ni mpuuzi namba moja! Ukipewa vitu viwili vibovu ina manisha ubovu wake utakuwa sawa? Hizi akili za kuvukia barabara nazo ni shida
Punguza povu,siku hizi hoja ni bunge live na kutetea mafisadi hamna jipya
 
Ndugai hafai kuwa hata mbunge,achilia mbali spika!Hivi ile kesi yake ya wakati wa uchaguzi ya kumpiga mtu na gongo kichwani mpaka akazimia imeishia wapi?
 
Back
Top Bottom