MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Wakuu sitaki niongee kishabiki wala kwa hisia ila tu naongea kiuhalisia kupitia jukwaa hili!
Nimejaribu kufanya ulingani wa maspika wa awamu zote zilizopita hasa baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa kwa kuwaangalia kina Pius Msekwa, Samweli Sitta na Anne Makinda na kulinganisha na Spika wa sasa mbunge wa Kongwa Mh Job Ndungai nakosa kabisa jibu ni wapi tunaelekea! Wasi wasi wangu ni kwamba kuna uwezekano wa bunge kukaa tena na kutafuta spika mwinge.
Nikiwaangalia maspika wote hao watatu waliopitia kwa kuzingatia ubobezi wa siasa za nchi hii, ubobezi wa masuala ya kisheria, ubobezi wa uongozi katika utumishi wa umma ukizingatia zaidi baadhi yao walikua mawaziri na wakuu wa mikoa katika serikali zilizopita.
Job Ndungai ni Afisa Wanyama pori na ndio taaluma yake hiyo, pamoja na kua na shahada ya sheria ya chuo kikuu huria lakini hiyo tu bado haitoshi kumpa uwezo wa kumudu changamoto za bunge hili lililojaa wabunge wa rika na jinsia tofauti, wasomi wa kada mbali mbali! Kwa hakika maji yakishamwagika hayazoleki lakini tukubaliane kua "He will suffer the most".
Uzoefu wa spika ndugai katika masuala ya kisiasa ni ubunge tu ukiachilia nafasi ya unaibu spika na uenyeketi wa kamati za bunge kumlinganisha na maspika hao wote watatu waliopitia ambao waliwahi kua maafisa wa ngazi za juu katika utumishi wa umma katika serikali zilizotangulia.
Nikimwangalia kwa jicho langu la kipee Ndungai hana uvumilivu hata kidogo hasa katika masuala ya kisisa! Hua ana hasira za karibu sana pindi inpotokea tofauti bungeni, napata shida sana kuridhika na uvumilivu wake hasa kwa kujaribu kuzikumbuka siku za nyuma alipokua naibu spika ambapo mara nyingi mambo yalikua yakiharibikia kwenye viganja vyake.
Hii nafasi ya uspika ilitakiwa apewe mtu aliye na uvumilivu wa hali ya juu, mtu mwenye uzoefu wa kutosha katika masuala ya siasa za nchi hii, mtu mwenye umri wa utu uzima usiokua na mihemko ya kisiasa na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kutafsiri kanuni na sheria bungeni kwa kuzingatia aina ya bunge lililopo, lakini kwakua tunapenda sana kutanguliza ushabiki usiokua na maana basi hatuna namna tukubaliane na hali hii tu.
Najaribu kufikiria wale ambao wanaweza kua washauri wakuu wa spika huyu nako bado nakosa kuridhika na timu iliyopo! Mfano nikimuangalia Naibu spika wake ndg Tulia Mwansasu msomi huyu wa sheria, lakini bado hana uzoefu wowote wa masuala ya kisiasa kutosha kua Mshauri wa spika Ndungai kwani masuala ya kisiasa kua msomi tu haitoshi na uzoefu ni sifa muhimu sana!
Nikijaribu kumwangalia Mwenyekiti Andrew Chenge ambaye pamoja na madhaifu yake yote upande mwingine lakini angalau hapa ndio kidogo kuna unafuu kutokana na uzoefu wake katika siasa za nchi hii na pia anao uwezo mkubwa sana kuzitafsiri kanuni na sheria mbali mbali za bunge,Lakini Swali langu juu ya Chenge ni kwamba Je, ule udhaifu wake hasa katika uadilifu una usalama wowote kwa ustawi wa bunge la spika Ndungai?
Nawasilisha na "mark my words"