Spika amuokoa Zitto kukamatwa na Police Bungeni

Baba Munah

Member
Feb 7, 2017
19
49
KITENDO cha Jeshi la Polisi kutaka kumkamata Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, juzi baada ya kutoka bungeni, kilimfanya mbunge huyo kuondoka bungeni usiku wa manane kuamkia jana kwa msaada wa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Juzi, wakati Zitto akiwasilisha hoja bungeni kuhusu utaratibu wa wabunge, hasa wa upinzani kukamatwa na polisi bila utaratibu, alibainisha kuwa hata yeye amepewa taarifa kuwa akitoka nje ya viwanja vya Bunge atakamatwa, kuahidi kulala bungeni ili kuwakwepa polisi.

Baada ya wabunge wa upinzani kususia kikao cha Bunge juzi saa 10:30 jioni kutokana na hoja hiyo kupingwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Zitto aliendelea kuwepo ndan ya eneo la Bunge hadi jana saa 6:25 usiku alipoondoka kwa msaada wa Ndugai aliyempatia usafiri.

Hata hivyo, kususia kikao kwa wabunge hao wa upinzani sambamba na Zitto kusakwa na polisi, jana asubuhi kulimfanya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kutaka Serikali na Bunge kufanya kazi kwa pamoja, huku akisema taarifa ya kukamatwa hovyo kwa wabunge ataifikisha kwa Ndugai aliyedai kuwa ataitolea tamko rasmi leo.

Zitto asimulia

“Niliondoka saa 6 usiku ikiwa ni baada ya mashauriano kati yangu na Katibu wa Bunge (Dk Thomas Kashilillah) na Spika Ndugai ambaye aliwasiliana na IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi-Ernest Mangu),” alisema Zitto.

“Nilivyokuwa nawasilisha hoja yangu bungeni nilikuwa najua kila kitu juu ya kukamatwa kwangu ndio maana nikaamua kutotoka bungeni kwani walikuwa wakinisubiri nje ya viwanja wa bunge.”

Alisema baada ya majadiliano ya muda mrefu, IGP aliwasiliana na Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa ambaye alibainisha kuwa mbunge huyo alikuwa akitafutwa kwa kutoa kauli uchochezi alipokuwa mkoani Shinyanga, kubainisha kuwa polisi ilikiri kutoona kosa lake.

Alisema baada ya mashauriano hayo alihakikishiwa kuwa akitoa hatokamatwa na polisi lakini kwa kujihami zaidi Spika Ndugai alituma usafiri wa kumchukua.

“Spika aliwasiliana na mkuu wa ulinzi wa Bunge ili kuniwezesha kutoka salama ila pamoja na kuwasiliana naye bado alinitumia gari ambalo lilinitoa ndani ya viwanja vya Bunge,” alisema.

Juzi mpaka saa tatu baadhi ya mageti ya kutoka na kuingilia ndani ya Bunge kulikuwa na magari ya polisi huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kwa kiwango kikubwa.

Kauli ya Mwenyekiti wa Bunge

Jana wakati akijibu mwongozo wa mbunge wa Tarime Vijijini(Chadema), John Heche kuhusu polisi kuwakamata wabunge bila utaratibu, Chenge alisema polisi wanaweza wasiwakamate wabunge pindi vikao vya Bunge vinapokuwa vikiendelea, badala yake kufanya hivyo wakati mwingine.

Katika maelezo yake, Chenge alisema kuna haja pia ya kuimarisha uhusiano kati ya Serikali na Bunge kwa kuwa mihimili hiyo ina majukumu yanayofanana.

“Heche nimekusikia ingawa hukueleza kwa undani, lakini najua suala hili lilianza jana na Naibu Spika akalitolea ufafanuzi,” alisema.

“Ushauri wangu katika hili, kuna haja ya kuwa na mahusiano mazuri kati ya Bunge na Serikali, lakini pia nakuomba Heche umwandikie Katibu wa Bunge umweleze mapendekezo yako ili yafikishwe katika Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa mjadala zaidi.

Alisema baada yah apo uongozi wa Bunge unaweza kujadiliana na Serikali kwa sababu kama polisi wanamhitaji mbunge, wanaweza kusema wa wakamkamata wakati mwingine kwa sababu wanajua anapoishi.

Awali, Heche alisema kama Bunge halitachukua hatua pindi wabunge wanapodharirishwa, utafika wakati Bunge litaanza kudharirishwa.

Alisema Bunge ni chombo kinachoheshimika duniani kwa sababu kinatunga sheria na kupitisha bajeti ya Serikali lakini hivi sasa heshima yake.

“Hii tabia ya wabunge kukamatwa ovyo, tena bila taarifa ya Spika, haipendezi na hata wakuu wa wilaya wanawanyanyasa sana wabunge huko majimboni. Kwa hiyo, naomba mwongozo wako mheshimiwa mwenyekiti ili uniruhusu niwasilishe hoja yangu ili Bunge liijadili,” alisema Heche.

Wabunge walivyotoka bungeni

Juzi, wabunge wa upinzani, walitoka nje ya Bunge wakionyesha kutoridhishwa na majibu ya Naibu Spika, Dk. Tulia Akson, aliyoyatoa wakati alipokuwa akijibu taarifa ya kukamatwa kwa wabunge wa upinzani iliyowasilishwa na Zitto.

Katika taarifa hiyo, Zitto aliwataja wabunge wa Chadema, Godbless Lema wa Arusha Mjini aliyeko mahabusu katika Gereza la Kisongo, Arusha kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali anayetumikia kifungo cha miezi sita katika Gereza la Ukonga Dar es Salaam na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, wakati Dk. Tulia akijibu taarifa hiyo, alisema kanuni za Bunge zinataka Spika wa Bunge apewe taarifa za kukamatwa mbunge aliyetenda makosa ya madai na kama siyo makosa ya madai, hakuna haja ya spika kupewa taarifa.

Chanzo: Mtanzania
 
... Kweli tumefanimiwa kujenga viwanda vya kuzalisha dawa ya kupambana na uchochezi... Akili zenu zoote ni kufikiri kwamba shida kubwa ya watanzania ni uchochezi...
Nendeni mkajibu na tuhuma za madawa ya kulevya polisi, mnatakaka viwanda na mnawageuza vijana wa Taifa hili kuwa mateja, hivyo viwanda vitaendeshwa na roboti?
 
Nendeni mkajibu na tuhuma za madawa ya kulevya polisi, mnatakaka viwanda na mnawageuza vijana wa Taifa hili kuwa mateja, hivyo viwanda vitaendeshwa na roboti?
... Majina ya mapapa wa madawa JK alishasema yapo magogoni, nyie mnahangaika na akina Chidibenzi na Ray C...
 
Watanzanzani sijui kama wali wengi wameelewa au wamelewa tuongeze na kimela maana dah akili nyingi zmekufa na ambae hajui hajui kama hajui.haya ni makosa yanayotokea kwenye nchi ama enzi za ukoloni dah Tanzania ya viwanda mi naota tu
 
Angalao spika anawasaidia wabunge wenzake waliochaguliwa na wananchi lakini yule mama aliyeteuliwa na Mwenyekiti wa ccm ni shida
 
Mungu ampe afya njema Ndugai arudishe heshima ya bunge.. angekuwa yule mama..looo angetaka kufunga bunge na funguo aende nazo kwake. Hongera Ndugai kwa upendo wako kwa wengine.
 
Bila ya Zitto kulianzisha hili Sokomoko Bungeni Jana ilikuwa Lissu nae aanze kutumiki Kifungo Kama cha Lema Ila ikaonekana aachwe this time isilete zogo zaid kwa kina Zitto
 
Lazima wabunge wajifunze kusema kwa kuzingatia misingi ya haki na sheria siyo mtu unatukana tu kisa mbunge.
 
Kuwa mwanasiasa maana yake sio kuwa na lugha za kejeli na matusi. Jenga hoja katika misingi isiyokuweka hatiani
Utajenga hoja kwa kufurahi kukamatwa kwa mtu kama mbunge ambaye ni public figure kama mbwa na isitoshe yuko kwenye majukumu yake ya kulitumikia taifa!!!!Uliwahi kujenga hoja kwa nini baadhi ya wabunge wanaitwa kwa kumwandikia barua speaker na wengine kuviziwa kukamatwa?Unajenga hoja ya nini na kwa nani?Haki huinua taifa ndugu!Mimi namkubali Rais sana na ninaamini watendaji kidogo wanateleza tu kwa sababu za uwoga
 
Utajenga hoja kwa kufurahi kukamatwa kwa mtu kama mbunge ambaye ni public figure kama mbwa na isitoshe yuko kwenye majukumu yake ya kulitumikia taifa!!!!Uliwahi kujenga hoja kwa nini baadhi ya wabunge wanaitwa kwa kumwandikia barua speaker na wengine kuviziwa kukamatwa?Unajenga hoja ya nini na kwa nani?Haki huinua taifa ndugu!Mimi namkubali Rais sana na ninaamini watendaji kidogo wanateleza tu kwa sababu za uwoga
Tunapenda kuwa na wanasiasa wa upinzani lakini upinzani uliopo sasa sio upinzani ni usanii.! Mbona katika bunge la Tisa upinzani walikuwa na hoja?! Kwanini leo hii wasikamatwe akina mnyika. Kwani wao hawakua kwenye kampeni? Siasa za marekani haziwezi kuwa zetu. Lets learn our way.!
 
Back
Top Bottom