Speed za magari barabarani

Speed za magari barabarani

The CIA

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2017
Posts
479
Reaction score
479
Habari wana jamii, poleni na majukum mliyonayo ya kuhakikisha mnasukuma gurudumu la maendeleo yenu na taifa kwa ujumla.

Naomba kurudi kwenye maada bila kukawia nisije nikasahau lengo la hii thread,

Hizi speed/mwendokasi wa gari barabarani hapa nchini ambao kwa kiasi fulani imekuwa chanzo cha mapato ya askari wetu wa usalama barabarani ipo ki sheria na kikatiba au ipoje ipoje,

Na kama speed wanazozipanga zipo kisheria
mfano
- kwenye mbuga za wanyama unakuta speed ni 50 mpaka 30 kwa saa,

- sehemu ya shule
- sehemu ya soko
- na sehemu zingine kulingana na mazingira yake utakuta speed ni 80 mpaka 50.
narudi tena kama speed hizo zipo kisheria

Viongozi wa serikali kama mawaziri, rais na wengine wengi haziwagusi na nikwanini? au wao wanaruhusiwa kuvunja sheria?

Kwa wao haiwahusu yaani wanaruhusiwa kuvunja sheria kwa nini sisi wananchi tugeuzwe kitegauchumi kwa jeshi la usalama barabarani?

Nashauri sheria hizi zituhusu wote, maana katiba inasema hakuna aliye juu ya sheria.. this is not fair.

Karibuni kwa
nyongeza, dukuduku, lawama na ushauri.
 
Daah!sasa hivi kumiliki gari ni dhambi kubwa sana, ukionekana barabarani afe kipa afe beki faini utalipa tu hata taa ya plate number isipowaka ni dhambi
 
Sikuhizi hawakagui hata magari badala yake wao huchukua pesa Tu.
 
Viongozi hapo umenena vyema hii ndio inatuletea na folen za ajabu ajabu mjini kisa kusafishiwa barabara ili wapite kwa speed ya 80kph. Wanakimbilia kwa kusema huo msafara wa mtu mzito
 
e42ced336eea5d475c7ddbe17453573c.jpg
 
Back
Top Bottom