gasto genaro
JF-Expert Member
- Oct 15, 2014
- 780
- 554
Tujadili muelekeo wa uchaguzi huo tunauonaje? Kwa mujibu wa matukio mbalimbali ya kisiasa nchini, unaona uchaguzi huu utakuwaje?Tu-discuss nn wakat hatujui hata majina ya wagombea???
Kwanini mkuuHuhitaji darubini Kali kutambua kuwa Hali ya CCM itakuwa tete
Kwanini umeyasema haya yote mkuu?UCHAGUZI KUELEKEA 2020 CCM ITASHINDA KWA KISHINDO .
PILI UCHAGUZI WA 2020 UPINZANI WATAANGUKA SANA KATIKA NGAZI YA UBUNGE NA UDIWANI.
TATU IDADI YA WAPIGA KURA WATAKAOJITOKEZA ITAKUWA NI NDOGO SANA
Mkuu kasema hili halipo ktk mipango yake.Ccm inashinda tu Ukawa hawawezi kushinda kwasababu wameshindwa kupingania katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Katiba mpya ni dhahiri kabisa haiwez kupatikana kwa sasa.1.Wapinzani tusijidanganye kabisa 2020 bila tume huru na katiba mpya CCM itashinda kwa zaidi ya 80%..... tukikosa tume huru bora tususe tu maana hata ubunge na udiwani tutaporwa hata haya majimbo tulionayo na tutaambulia machache sana......
2. Pili tuhakikishe tunalazimisha serikali iheshimu sheria ya vyama vya siasa kma mwaka 2017 utaisha na mikutano imezuiwa huku kwenye majukwaa anaonekana magufuli tu then kwan namna yoyote ile 2020 hatutoambulia chochote. Hata kma watatupa tume huru ila kma mikutano ya kukagua uhai wa chama hairuhusiwi watanzania hasa wa vijijini watatusahau na hivyo nguvu zote zile za M4C na operation sangara vitakuwa ni wastage of time.
3. Tuwekeze nguvu majimbo tulionayo na ambayo tunataka tuyachukue kwa jinsi magu alivyo sioni kma NEC inaweza mtangaza mpinzani mshindi nafasi ya rais hta kma tutamsimamisha OBAMA...... tujijenge kwenye halmashauri na majimbo tulionayo itakuwa kampeni tosha kwa ajili ya 2020.
MUHIM NI TUME HURU NA MIKUTANO KWANZA
Sawa katiba mpya haiwezekani maana dikteta kaamua kuipa kisogo..... solution ni minimal reforms kma ilivyokubaliwa kati ya serikali iliopita na TCD.... bunge maalum liitishwe ili lipitishe hizo minimal reforms zitakazozaa tume huru, mgombea binafsi,matokeo ya urais kupingwa mahakamani, vyama kuungana n.kKatiba mpya ni dhahiri kabisa haiwez kupatikana kwa sasa.
Hapa wapinzani watafute plan B labda
Salaam wakuu,
Ni mapema mno kuanza kuzungumzia uchaguzi mkuu ujao 2020, lakini pia siyo vizuri kuchelewa sana kuzungumzia suala hili, ikiwa ni pamoja na kujiandaa.
Mawazo yako hapa pengine kwa namna moja au nyingine yanaweza kuonesha mwelekeo wa uchaguzi huu mkuu ujao.
Unachotakiwa kufanya, ni kuelezea mtazamo wako kuhusu namna unavyohisi uchaguzi huu utakavyokua.
Unaweza pia kueleza ni unahisi ni nani ataibuka kidedea na kwanini.
Unaweza kueleza pia unahisi ni nani atakayeshindwa na kwa nini.
Unaweza pia kueleza ni mabadiliko gani ungependa yafanyike ili kuufanya uchaguzi huu mkuu ujao uwe murua kushinda zilizopita.
Katika hili, tuweke itikadi zetu za vyama vya siasa na tujadili kama WATANZANIA.
Tuendelee kujadili kila leo kulingana na matukio mbali mbali yanayotokea nchini ambayo tutahisi kwa namna moja au nyingine yataathiri upande fulani ktk uchaguzi ujao 2020.
Tukijadili hadi 2020, basi itasaidia kuona mwelekeo mzima wa uchaguzi huo kwa mawanda mapana.
Karibuni..
Mkuu, hivi kwako wewe 2020 ni mbali?Fanya kazi wewe ujenge maisha yako na wanaokutegemea, ndo kwanza tumemamliza uchaguzi unawaza uchaguzi mwingine? Si uhamie Kenya tayari wako kwenye campaign mode!